Sibuka FM

TAWA yavuna viboko wawili, watoa kitoweo kwa wananchi Busega

20 November 2024, 8:43 pm

Kwenye picha ni afisa wanyamapori mwandamizi kutoka pori la akiba la Kijereshi, Rogathe Wado akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani baada ya kufanikisha uvunaji wa Viboko wawili Picha na Daniel Manyanga

Usalama wa raia ni ajenda ya kwanza katika Taifa lolote hatuwezi kuzungumzia maendeleo wakati huo raia wake wanapitia changamoto za kiusalama wao na mazao hasa waishio kandokando ya mapori au hifadhi.”

Na, Daniel Manyanga

Viboko wawili waliokuwa wanahatarisha usalama wa wananchi na mali zao kwenye kata ya Kabita wilayani Busega mkoani Simiyu wameuliwa na Mamlaka ya Usimamizi wa wanyamapori Tanzania (TAWA) ikiwa ni zoezi la uvunaji la wanyama hatarishi katika jamii.

Kwenye picha ni mmoja wa wananchi wa kata ya Kabita , Rahel Nicholaus akizungumza namna ambavyo wanyama hatari walivyokuwa kero katika utendaji kazi wao Picha na Daniel Manyanga

Ng’oga Genda na Rahel Nicholaus wakazi wa Kabita wakizungumza na Sibuka fm wameomba zoezi hilo liwe endelevu ili waweze kufanya shughuli zao ikiwemo kilimo bila hofu yoyote ya wanyama hatari wanaokwamisha utendaji wa shughuli za kiuchumi kwa kuhofia usalama wao na mazao yao.

Sauti za wananchi wakipongeza hatua ya TAWA kufanikisha uvunaji huo ambao ulikuwa ni changamoto hasa wakati wa kilimo

Michael Mabula ni mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM kata ya Kabita ameipa kongole serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori (TAWA) kwa hatua hiyo ya kupunguza wanyama walio hatari.

Sauti ya mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM kata ya Kabita, Michael Mabula akitoa pongezi kwa TAWA kufanikisha uvunaji huo
Kwenye picha ni mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM kata ya Kabita, Michael Mabula akizungumza kufuatia zoezi la uvunaji wa wanyama hatari.

Akizungumzia ufanikishaji wa zoezi hilo afisa wanyamapori mwandamizi wa mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori (TAWA) pori la akiba la Kijereshi,Rogathe Wado amesema kuwa uvunaji wa wanyama wanaohatarisha maisha na mali za watu utakuwa endelevu.

Sauti ya afisa wanyamapori mwandamizi kutoka pori la akiba la Kijereshi, Rogathe Wado akizungumzia zoezi la uvunaji huo
Pichani ni mmoja wa Kiboko aliyeuliwa na mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori TAWA katika kata ya Kabita Picha na Daniel Manyanga