Sibuka FM

Kipindupindu ni zaidi ya vita Simiyu, Amref watia nguvu

19 November 2024, 8:53 pm

Muonekano wa picha ikionesha uzinduzi wa mradi wa afya thabithi Picha kutoka maktaba ya Sibuka fm

Adui wa maendeleo ni maradhi hatuwezi kufanya kazi za kiuchumi wakati huo wananchi wanachangamoto ya kiafya hivyo jukumu letu ni usalama kwanza wa raia”.

Na, Daniel Manyanga

Shirika la Amref  Heath of Africa chini ya mradi wa Afya Thabithi unatekelezwa kwa kushirikiana na Shirika la Tanzania Communication Development Center (TCDC) limewataka wananchi wilayani Bariadi mkoani Simiyu kuendelea kujikinga na mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu ambao umeukumba mkoa huo.

Picha ikionesha uzinduzi wa mradi wa afya thabithi mkoani Simiyu picha ni kutoka maktaba ya Sibuka fm

Akizungumza na Sibuka fm wakati akitoa elimu ya kujikinga na ugonjwa wa kipindupindu afisa elimu ya mabadiliko ya tabia kutoka shirika la Tanzania communication development center (TCDC ) mkoani Simiyu,Antony Nakasenga amesema kuwa ili kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa huo wananchi wanapaswa  kuepuka kunywa maji yasiyo salama, kutumia vyombo safi na kuhakikisha wanakula chakula kilichoandaliwa katika mazingira safi pamoja na matumizi ya vyoo.

Sauti ya afisa elimu ya mabadiliko ya tabia, Anthony Nakasenga akitoa elimu ya kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa kipindupindu haswa kwa wananchi

Kwa upande wake mhamasishaji wa maswala ya mabadiliko ya kitabia katika jamii mkoani wa Simiyu,Maria Masanzu amewataka wananchi kuhakikisha wanawapitia huduma ya kwanza kwa wagonjwa ikiwemo kuwatengenezea Glucose ama olo endapo kama kuna mtu katika familia ataonekana kuwa na dalili moja wapo kati ya Kuhara na Kutapika bila tumbo kuuma na baada ya hapo wampekeke katika vituo vya afya au hospitali kwa matibabu zaidi.

Sauti ya mhamasishaji wa elimu ya mabadiliko ya tabia katika jamii,Maria Masanzu akitoa maelekezo ya namna ya kumpatia huduma ya kwanza kwa mgonjwa wa kipindupindu kabla ya kumpeleka vituo vya afya

Kipindupindu ni ugonjwa wa kuambukizwa unaosababishwa na bacteria aina ya Vibrio Cholera kupitia maji machafu au chakula kichafu(kula mavi mabichi).

Muonekano wa picha katika maeneo yanayoweza kuchangia kuambukizwa kwa ugonjwa wa kipindupindu katika jamii yetu Picha kutoka maktaba ya Sibuka fm