Maswa: Zaidi ya milioni 300 kunufaisha wanawake, vijana na walemavu
12 November 2024, 4:52 pm
“Katika kupambana na umasikini nchini kupitia asilimia kumi ya mapato ya ndani ya halmashauri kundi la wanawake,vijana na watu wenye ulemavu wameendelea kunufaika kiuchumi.”
Na, Daniel Manyanga
Zaidi ya milioni miatatu zitokanazo na makusanyo ya ndani zimetangwa na halmashauri ya wilaya ya Maswa mkoani Simiyu katika kuendelea kuinua kipato kwenye makundi ya Kinamama,Vijana na Watu wenye ulemavu kwa kuwakopesha kwa bila riba.
Akizungumza na Sibuka Fm mkuu wa division ya maendeleo ya jamii wilayani Maswa,Rodgers Lyimo amesema kuwa halmashauri hiyo imetenga kiasi Cha milioni miatatu kumi na nne zitokanazo na makusanyo ya ndani ili kuweza kuwakopesha Wanawake,Vijana na watu wenye Ulemavu kupitia vikundi ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Lyimo amesema kuwa fedha zitatokana na asilimia Kumi ya makusanyo ya ndani ya halmashauri inapaswa kupelekwa katika makundi matatu Wanawake asilimia 4,Vijana asilimia 4 na Watu wenye Ulemavu asilimia 2.
Rodgers Lyimo ameongeza kuwa vikundi vyote vinapaswa kuomba upya kutokana na kanuni ,sheria na muongozo kuwa mipya hivyo vikundi viombe kuanzia ngazi ya kata huku akitaja vigezo vya vikundi Ili Kupata huo mkopo.
Lucia Misinzo ni afisa maendeleo ya jamii wilayani hapo amesema kuwa maombi ya mikopo yameshaanza kupokelewa ngazi ya kata ili kamati za mikopo za kata ziweze kutoa maelekezo kwa wakopaji huku kundi la vijana likionekana kupendelewa kuanzia miaka kumi na nane hadi arobaini na tano wanakopesheka.