Sibuka FM

Wanafunzi Masela sekondari wafundwa  elimu ukatili wa kijinsia

24 October 2024, 11:04 pm

Pichani:Kushoto ni Madam,Kashidye Mshila,akifuatiwa na Mkurugenzi wa (JACCAFO)Joseph Ngeleja,akifuatiwa na Emmanuel Cosmas mwenye kofia na kulia mwisho ni Makamu Mkuu Masela Sec,School.Picha na Alex Sayi.

Jamii ya watanzania imeendelea kukumbushwa kuchukua tahadhari juu ya matukio ya ukatili wa kijinsia,kwakutoa taarifa nakuendelea kuwaelimisha watoto walio majumbani na wanafunzi ili kuwanusuru watoto hao na athari za ukatili wa kijinsia.

Na,Alex Sayi.

Wanafunzi wa shule ya sekondari Masela iliyopo kijiji na kata ya Masela wilayani Maswa Mkoani Simiyu  wamepatiwa elimu juu ya ukatili wa kijinsia na athari zake kutoka shirika la Juniors and Child Care foundation (JACCAFO)

Elimu hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa shirika hilo,Bw,Joseph Ngeleja  wakati akizungumza na wanafunzi hao,baada yakudhuru shuleni hapo,Oct,21,mwaka huu kwa lengo la kutoa elimu ya ukatili wa kijinsia.

Sauti ya Mkurugenzi wa (JACCAFO)Joseph Ngeleja Jidayi

Awali Mkurugenzi huyo akizungumzia wasifu wa Shirika hilo amesema kuwa shirika hilo limejikita kusaidia watu wenye ulemavu,watoto waishio kwenye mazingira magumu,wanawake na wazee.

Sauti ya Mkurugenzi wa (JACCAFO)Joseph Ngeleja Jidayi
Pichani:Aliyesimama ni Mkurugenzi wa (JACCAFO)Joseph Ngeleja.Picha na Alex Sayi.

Emmanuel Cosmas mwanachama wa Shirika hilo  akizungumza na wanafunzi hao amewataka wanafunzi hao kutoa taarifa za ukatili wa kijinsia nakujiepusha na tamaa za muda mfupi.

Sauti ya Emmanuel Cosmas Mwanachama wa (JACCAFO)
Pichani:Aliyesimama ni Emmanuel Cosmas.Picha na Alex Sayi

Kwa upande wake kaimu mkuu wa shule hiyo Msafiri Mageuza alimshukuru Mkurugenzi wa shirika hilo kwakufika nakutoa elimu hiyo shuleni hapo.

Sauti ya Makamu Mkuu wa Masela Sec,School.
Pichani:Aliyesimama ni Makamu Mkuu wa Masela Sec,School,Mwl,Msafiri Mageuzi.Picha na Alex Sayi.

Aidha Claudia Macha na Benedicto Gitambi Gagagaga wakizungumza na Sibuka fm wamesema kuwa masuala hayo ya ukatili wa kijinsia yamekuwa na athari kwenye jamii hasa kwa watoto wa kike.

Sauti ya Claudia na Benedicto wanafunzi wa Masela Sec,School
Pichani:Ni Claudia Macha mwanafunzi wa Masela Sec,School.Picha na Alex Sayi
Pichani:Wanafunzi wa Masela Sec,School wakiwa na furaha baada ya kukabidhiwa baadhi ya zawadi na Mkurugenzi wa(JACCAFO)ikiwemo,Sale za shule,Viatu,Taulo za kike na Madaftari.Picha na Alex Sayi.