Sibuka FM

Wananchi Maswa walalamikia umeme kufika maeneo ya mijini tu

27 September 2024, 11:06 pm

Pichani Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu ambaye hayupo Pichani katika mkutano wa Hadhara wa Kusikiliza Kero za Wananchi. Picha na Nicholaus Machunda

Unakuta meme umefika maeneo ya sentani tu halafu sisi tuliopo pembezoni hatupati tunaambiwa tu mradi unaishia hapo kwani sisi wa pembezoni hatustahili kupata huduma ya umeme?

Wananchi wa kijiji cha Mwakabeya   kata  ya  Ipililo  Wilayani  Maswa  Wamelalamikia Huduma  ya  Umeme  kufika  kwenye  Senta  tu   na   wengine  waliopo  Maeneo  ya  Pembezoni  kukosa  Nishati  hiyo  Muhimu.

Wakitoa  Kero  hiyo  Mbele  ya  Mkuu  wa  Mkoa   wa  Simiyu  Mhe  Kenani  Kihongosi   baadhi  ya  wananchi hao  Maduhu  Tungu  na  Dogani  Ndoma  Lyabita  wakapaza  sauti  zao   na  kuomba  kusaidiwa  ili  nao  wanufaike

Sauti za Wananchi wa kata ya Ipililo wakielezea changamoto ya Umeme

Akitoa  Majibu  kuhusu  Changamoto  hiyo  Meneja  Tanesco  Mkoa  wa  Simiyu  Alistidia Clemence  Kashemeza amekiri  kuwepo  Changamoto  hiyo  na kuahidi  kukamilisha  maeneo  ambayo  hayajafikiwa  na  Nishati  ya  Umeme  huku  akiwataka   Wananchi  kulinda  na  kutunza  Miundombinu   hiyo  kwani Serikali inatumia  gharama  kubwa   kuwafikia.

Sauti ya Meneja Tanesco Mkoa wa Simiyu akitoa Ufafanuzi kuhusu Umeme
Pichani ni Meneja Tanesco Mkoa wa Simiyu akitoa Ufafanuzi kuhusu Umeme

Kenani  Kihongosi  ni  Mkuu  wa  Mkoa  wa  Simiyu  amesema  kuwa  Serikali  inafanya  kazi  kubwa  kuhakikisha  wananchi  Wanasogezewa  Huduma  mbalimbali  ikiwemo  Suala  la  Umeme   hivyo  wawe  na  subira  katika   kuiamini  Serikali  kuwa  itawaletea  huduma  hiyo.

Sauti ya RC Kihongosi akitoa ufafanuzi kuhusu hoja za Wananchi

Mhe  Kihongosi  ameongeza  kuwa katika  Siasa ni  vizuri  kuvumiliana  na Kupendana  na  siyo kuleta  chuki  zitakazopelekea  kuharibu  Amani  tuliyonayo  kwani  kuna  Maisha  baada  ya  Siasa

Sauti ya RC Kihongosi akizungumzia kuhusu Siasa za chuki