Wananchi Maswa watoa Maoni kuhusu Dira ya Maendeleo 2025- 2050
15 August 2024, 10:40 am
Wananchi Wilayani Maswa Mkoani Simiyu wamepaza sauti zao na kutoa Maoni juu ya Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025 – 2050 wakati wa Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya – DCC kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo.
Wamesema kuwa katika Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025 – 2050 Serikali iboreshe katika Huduma za Afya, Kilimo, Mifugo, Elimu na Miundombinu ili kukuza uchumi wa Taifa.
Katika kikao hicho kilichohusisha wadau mbali mbali wakiwemo Viongozi wa Dini nao pia wakasisitiza Suala la Amani na Utulivu katika Nchi ili kukuza Ustawi wa Taifa
Akifungua kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe Aswege Kaminyoge amesema kuwa Katika Utekelezaji wa Dira Serikali imefanya Mambo makubwa ya Maendeleo kwa Wananchi katika nyanja mbali mbali ikilinganisha na miaka ya zamani kabla ya Dira
Emmanuel Ludomya ni Mratibu wa Dira ya Maendeleo ya Wilaya ya Maswa akasema maoni yaliyotolewa na Wananchi watayafikisha sehemu husika ili Serikali iyafanyie kazi kwa Maendeleo ya Taifa.