Madereva wazembe,vyombo vibovu hakuna atakae kuwa salama Simiyu
19 July 2024, 5:29 pm
“Katika kuzuia na kupambana na madereva wazembe wanaosababisha ajali zisizo za lazima zinazotokana na ubovu wa vyombo vya usafirishaji wanavyotumia jeshi la polisi mkoa wa Simiyu limekuja oparesheni la ukaguzi wa vyombo vya moto”
Na,Daniel Manyanga
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Simiyu kamishina msaidizi wa polisi ACP.Edith Swebe ametoa rai kwa madereva wa vyombo vya moto mkoani hapo kuhakikisha wanapeleka vyombo vyao vya moto kwenda kukaguliwa na jeshi la polisi ili kuepusha ajali ambazo siyo za lazima zinazotokea kwa kusababishwa na ubovu wa vyombo wanavyovitumia.
Kamanda ACP, Edith Swebe ametoa rai hiyo wakati akizungumza na madereva hao katika uzinduzi wa zoezi la ukaguzi wa vyombo vya moto mkoani Simiyu, uliofanyika mjini Bariadi na kuwataka madereva hao kuhakikisha vyombo vyao vinakaguliwa.
Kwa upande wake mkuu wa usalama barabarani mkoa wa Simiyu SSP. Philbert Rwomunshaka amesema kuwa zoezi limeanza toka Julai 16 na litaendelea kwa muda wa miezi mitatu.
Nao baadhi ya madereva wa vyombo vya moto mkoani Simiyu wakaomba jeshi la polisi liendelee kuwapa elimu ili kuzuia ajali zinazoweza kuepukika.