DC Maswa aagiza viongozi, watendaji kusikiliza kero za wananchi
13 March 2024, 11:35 am
Mkuu wa Wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu Mh Aswege Kaminyoge ametoa maagizo kwa watendaji na viongozi wengine kusikiliza kero za za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi na siyo kusubiri viongozi wa ngazi za juu kuja kusikiliza kero ambazo zingetatuliwa na viongozi hao.
Mh Kaminyonge ametoa maagizo hayo leo katika mkutano wa hadhara wa wananchi wa wakati wa kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi ili wananchi waendelee kuiamini serikali yao chini ya Mh Rais Samia Suluhu Hassan.
Aidha mkuu huyo wa wilaya amewataka wazazi na walezi kuchangia chakula cha watoto shuleni ili wapate chakula shuleni wawe na uwezo wa kusoma vizuri kwani tafiti zinaonesha watoto wanaokula shuleni wana nafasi kubwa ya kufanya vizuri katika masomo yao ya darasani.
Katika kusikiliza kero za wananchi, kero ya maji ya kunyweshea mifugo likaibuliwa na mwananchi Mahira Miteko ambapo kaimu mtendaji wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mjini Maswa (Mauwasa) Raphael Mwita amesema watafuatilia ndani ya siku 7 ili kuondoa adha hiyo kwa wananchi