Mpango uboreshaji matumizi ya ardhi, milki kuondoa migogoro ya ardhi Maswa
14 July 2023, 9:14 am
Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi na Mpango wa Matumizi bora ya Ardhi Wilayani Maswa, Mkoani Simiyu Utaenda kuondoa Changamoto ya Migogoro ya Ardhi kwa Wananchi
Na Nicholaus Machunda
Imeelezwa kuwa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi na Mpango wa Matumizi ya Ardhi Wilayani Maswa, Mkoani Simiyu Utaenda kuondoa Changamoto ya Migogoro ya Ardhi kwa Wananchi.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe Aswege Kaminyoge Wakati wa Mkutano Mkuu wa Wadau wa Kujadili Mpango wa Matumizi bora ya Ardhi uliofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Maswa.
Imaculatha Senje ni Mkurugenzi Msaidizi wa Mipango miji na Vijiji kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi amesema kuwa Wizara imekusudia kupima vijiji zaidi ya Mia moja na kutoa Hati Miliki za Kimila Wilayani Maswa hali itakayosaidia kupunguza kero na Migogoro inayotokana na matumizi ya Ardhi.
Insert 02 Imaculatha Senje –Wizara ya Ardhi
Wabunge wa Majimbo ya Maswa Mashariki na Magharibi, Mhe Stanslaus Nyongo na Mhe, Mashimba Ndaki wameipongeza Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe Rais Samia kwakuleta Mradi huo utaoenda kuondoa Migogoro na Mauaji ya ndugu na wana ukoo wakigombania Mipaka ya Ardhi.
Baadhi ya Wadau walioshiriki katika Kujadili mpango huo wa Matumizi Bora ya Ardhi ni viongozi wa Dini, Wazee maarufu, Madiwani na viongozi wa taasisi mbalimbali wakapata nafasi ya kutoa maoni yao kuhusu mradi huo wa Upimaji wa ardhi na utoaji wa Hati miliki za kimila.
Naye afisa Mipango miji mkuu kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Aristides Mulokozi amesema kuwa mradi huo utagharimu zaidi ya Shilingi Bilioni mia tatu na arobaini na tano kwa Nchi nzima huku Wilaya ya maswa ikitarajia kutumia zaidi ya Bilioni tatu