Waziri Ummy: Sitarajii kusikia wananchi wanalalamikia dawa
13 July 2023, 4:02 pm
Serikali mkoani Simiyu kuendelea kuboresha utoaji wa huduma za afya ili kupunguza malalamiko ya wananchi na wagonjwa mkoani hapa.
Na Alex Sayi
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa hatarajii kuona wananchi na wagonjwa wakilalamikia uhaba wa dawa kwa kuwa bajeti imeongezwa toka Sh. Mil 244 hadi kufikia Sh. Bill 1 wilayani hapo.
Ummy ameyasema hayo wakati akizungumza na wauguzi wa afya wilayani Maswa akiwa ziarani mkoani Simiyu ziara iliyolenga kukagua na kujionea utoaji wa huduma za afya na miundombinu ya afya wilayani hapa.
Sauti ya waziri Ummy Mwalimu.
Mkuu wa wilaya ya Maswa Aswege Kaminyoge akitoa taarifa kwa Ummy Mwalimu akiwa ofisini kwake amesema kuwa wilaya hiyo ina jumla ya wafanyakazi wa Idara ya Afya 321 na ina upungufu wa watumishi 505 sawa na 61% .
Sauti ya Mkuu wa Wilaya Maswa Aswege Kaminyoge
Kwa upande wake, Stanslaus Nyongo mbunge wa jimbo la Maswa Mashariki amemuomba waziri Ummy kuridhia uboreshaji wa jengo la (RCH) ili kuwasaidia watoto wanaopata huduma kwenye hospitali hiyo.
Sauti ya Mhe. Stanislaus Nyongo (MP) Jimbo la Maswa Mashariki
Mkuu wa mkoa wa Simiyu Yahaya Nawanda amemshukuru rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia zaidi ya Sh.Bil 2.9 kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu mkoani hapa.
Sauti ya Dkt. Yahaya Nawanda.