Wanaoishi maisha duni hatarini kupata ugonjwa wa kifua kikuu
21 March 2023, 12:47 pm
Imeelezwa kuwa Jamii inayoishi katika Makazi Duni ipo hatarini kuugua Ugonjwa wa Kifua kikuu kutokana na hali zao za Maisha na Mfumo wa Maisha wanayoishi..
Hayo yameelezwa na Mratibu wa Mapambano dhidi ya Kifua Kikuu kutoka Muungano wa Wadau wa Kupambana na Kifua Kikuu Tanzania Nelson Terekela Wakati wa Mafunzo ya Kuwajengea Uwezo waandishi wa Habari wa Mkoa wa Simiyu kuhusu Ugonjwa wa Kifua kikuu na Matibabu yake.
Nelson amesema kuwa mara nyingi watu wenye makazi Duni miundo mbinu ya Mzunguko wa Hewa na Mwanga wa kuingia na Kutoka unakuwa haupo hali ambayo inaweza kupelekea kuambukizana kama mmoja wenu ana Ugonjwa wa Kifua kikuu.
Emmanuel John ni Mratibu wa Kifua kikuu na Ukoma Mkoa wa Simiyu amesema kuwa Mkakati wa Mkoa ni kuwatafuta na Kuwaibua wagonjwa ambao hawajabainika na kuwaweka kwenye Matibu ili wasiendelee kuambukiza watu wengine kwani Ugonjwa wa Kifua kikuu huambukizwa kwa njia ya Hewa.
Aidha kwa Upande wake Mratibu wa Kitaifa wa Masuala ya Uraghbishi, Mawasiliano na Uhamasishaji kutoka Mpango wa Taifa wa Kifua kikuu na Ukoma Ndugu Julias Mtemahanji amesema kuwa lengo ni kuelekea katika Maadhimisho ya siku ya kifua kikuu ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh, Kasimu Majaliwa.
Baadhi ya waandishi walioshiriki Mafunzo hayo Samweli Mwanga na Annastazia Paul wamesema kuwa watatumia kalamu na Taaluma zao katika kuielimisha Jamii kuhusu Ugonjwa wa TB na namna ya kukabiliana na Ugonjwa huo.