Bilioni 440 kumtua mama ndoo kichwani Simiyu
6 November 2024, 5:48 pm
“Uhai ni maji na wanasayansi wanasema robo tatu ya dunia na mwili wa binadamu ni maji kwa kulitambua hilo wananchi waipongeza serikali kwa miradi ya maji”.
Na, Daniel Manyanga
Wananchi mkoani Simiyu wanaopata maji kwa kusuasua kutokana na kukosa vyanzo vya uhakika vya maji wameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa tenki katika mradi wa maji wa ziwa Victoria unaogharimu kiasi cha shilingi bilioni 440 na hivyo kunufaisha wananchi wa mkoani hapo.
Hatua hiyo imekuja mara baada ya bodi ya wakurugenzi ya mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Bariadi (BARUWASA) kufanya ukaguzi na kujionea maendeleo ya ujenzi wa matenki makubwa yanayohifadhi jumla ya lita milioni tano kufikia hatua ya umaliziaji kwa ajili ya usambazaji wa mabomba kuunganisha huduma hiyo.
Mhandisi Musalika Masatu ni mkurugenzi wa mamlaka ya maji na usafi wa mazingira mji wa Bariadi (BARUWASA) amesema kuwa kukamilika kwa mradi huo kutaenda kuongeza upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi mjini hapo
Melkizedeck Humbe ni mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Bariadi (BARUWASA) hapa akatoa maelekezo haya.
Mradi wa maji ya ziwa Victoria utahudumia wilaya za Busega,Bariadi,Maswa,Itilima na Meatu pale utakapokamilika.