Wananchi wilayani Maswa Mkoani Simiyu walalamikia upatikanaji wa huduma za Afya katika Hospitali ya Wilaya .
15 July 2021, 12:35 pm
Mkuu wa mkoa wa simiyu Mh Davidi Zacharia Kafulila amemuagiza mkuu wa Wilaya ya Maswa Mh , Aswege Kaminyoge Kufuatilia Changamoto ya mama wajawazito wanaoenda kujifungua katika Hospitali ya wilaya ya Maswa kutozwa Fedha.
Maagizo hayo ameyatoa wakati wa Mkutano wa hadhara wenye lengo la kusikiliza Kero za wananchi Uliofanyika katika Uwanja wa madeko uliopo mjini Maswa.
Mh, Kafulila amesema kuwa moja ya maeneo yanayokera ni Idara ya Afya hasa hospitali ya wilaya ya Maswa ambayo imekuwa ikilalamikiwa na wananchi kwa utoaji wa huduma duni ikizingatiwa hospitali hiyo inategemewa na wakazi wengi wa mji wa Maswa.
Akipokea maagizo hayo mkuu wa wilaya ya Maswa Mh Aswege Kaminyoge amesema kuwa tayari baadhi ya changamoto za upatikanaji wa Dawa ameshazifanyia kazi kwa kutoa maelekezo ya kupewa Orodha ya dawa zinazopatika kila siku..
Akitoa ufafanuzi kuhusu kulipishwa Fedha mama wajawazito, Mganga mkuu wa wilaya Dokta Mpolo Adorati amesema kuwa huduma za mama na mtoto zinatolewa Bure lakini kuna baadhi ya vipimo ambavyo mgojwa anapaswa kulipia..
Wakitoa malalamiko mbele ya mkuu wa Mkoa baadhi ya wakazi wa Maswa wamesema kuwa kuwekuwepo na changamoto katika huduma za Afya katika hospitali hiyo ikiwemo mama wajawazito kutozwa Fedha wakati wa kujifungua .
Hapa chini ni picha mbalimbali za mkutano huo wa hadhara.