NEC: Maafisa waandikishaji wasaidizi ngazi ya kata wala kiapo Maswa
29 August 2024, 8:13 pm
Kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa na Uchaguzi Mkuu 2025,Tume huru ya taifa ya uchaguzi imeendelea na zoezi la utoaji wa mafunzo kwa maafisa waandikishaji ngazi ya jimbo,maafisa waandikishaji wasaidizi ngazi ya jimbo na maafisa waandikishaji wasaidizi ngazi ya kata kwa Mikoa ya Simiyu,Mara na Manyara.
Maafisa waandikishaji wasaidizi ngazi ya kata Wilayani Maswa Mkoani Simiyu hatimae rasmi wamekula kiapo cha usimamizi wa zoezi la uandikishaji kuelekea uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.
Maafisa hao wamekula kiapo hicho mbele ya Enos Slyvester Missana hakimu mkazi mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Maswa Mkoani hapa wakati wa mafunzo kwa maafisa hao yaliyofanyika kwenye ukumbu wa Halmashauri Wilayani hapa.
Missana akizungumza na maafisa hao amesema kuwa wanapaswa kukiheshimu kiapo hicho ili wasiweze kupatikana na makosa ya kisheria kwa kukiuka kiapo chao.
Awali akifungua mafunzo kwa maafisa hao mgeni rasmi wa mafunzo hayo na afisa uandikishaji ngazi ya jimbo Wilaya ya Maswa Mashariki na Maswa magharibi,Maisha Mtipa amewataka maafisa hao kusimamia kwa weredi utekelezaji wa zoezi hilo.
Kwa upande wake Afisa Uhamiaji Wilayani hapa Constable Hashim Hamady,mbali yakutoa elimu ya Uraia kwa maafisa hao,lakini pia aliwaasa maafisa hao kutoa taarifa endapo watabaini uwepo wa raia wa kigeni wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo.
Aidha akitoa salamu za tume huru ya taifa ya uchaguzi mjumbe wa tume hiyo Bi,Magdalena Rwebangira amesema kuwa maafisa hao wa tume wanazungua kuhakikisha kuwa wanasimamia zaoezi hilo kikamirifu.