Sibuka FM

Tamasha la utalii, utamaduni Kanda ya Ziwa  lazinduliwa Simiyu

6 July 2024, 9:56 am

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Dunstan Kitandula akitazama Wasukuma wakicheza na Nyoka katika Uzinduzi wa Tamasha la Utamaduni Wilayani Bariadi, Simiyu Picha na Nicholaus Machunda

Kila kabila wana utamaduni wao, wasukuma wana utamaduni wao pia, ni vema kila kabila likaenzi utamaduni wake unasaidia katika Kulinda maadili na kukuza uchumi wa Taifa kupitia Utalii “Dunstan Kitandula ” Naibu waziri wa Maliasili na Utalii

Tamasha  la Utali  na  Utamaduni   Kanda  ya  Ziwa  limezinduliwa  rasmi  Wilayani  Bariadi  Mkoani  Simiyu  likiwa  na  lengo  la  kudumisha  na  kuenzi  Mila, tamaduni   na Desturi za   kabila la  Wasukuma

Akizungumza   wakati wa   Uzinduzi   wa Tamasha hilo   Naibu  Waziri  wa  Maliasili  na  Utalii   Mhe  Dunstan  Kitandula  amesema   ni  Muhimu  kuenzi  tamaduni   zetu   na  kuchochea  ukuaji wa  Uchumi  kupitia  utalii.

Sauti ya Dunstan Kitandula – Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii

Magesa  Nyambeho  ni  Afisa  Utamaduni  Mwandamizi   kutoka  Wizara  ya  Utamaduni, Sanaa  na  Michezo amesema  kumekuwepo  na  Mmomonyoko  wa  Maadili  katika  Jamii  hivyo  Serikali  imeandaa  muongozo  wa  Maadili  kwa  Wasanii  ambao  ndio  imekuwa  kichocheo  kikubwa.

Sauti ya Magesa Nyambeho- Afisa Utamaduni mwandamizi- Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo

Kwa  Upande  wa  Wandaaji  wa  Tamasha    hilo  Kilimanjaro  One  Tour  and  Travel  kupitia  kwa  Mkurugenzi  Mtendaji  Bi  Christina  Jengo  amesema  kuwa Tamasha  hilo  limelenga  kukuza  Utamaduni  wa  Kabila  la  Wasukuma  .

Sauti ya Christina Jengo- Mkurugenzi wa Kilimanjaro One Tour and Travel
Naibu waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Dunstan Kitandula akifurahia na Wacheza Ngoma wa kabila la Wasukumu wakati wa Uzinduzi wa Tamasha la Utalii

Naye  Mwenyekiti  wa  Utamaduni  Mkoa   wa  Simiyu    Buhimila   Shala  amesema  kuwa  ni  vyema  watu  wakajua  Utamaduni  wa  Kisukuma  siyo  Uchawi  na  kuiomba  Serikali  iwaunge  Mkono  katika  kuendeleza   na  Kuenzi  Mila  na  Utamaduni  wetu.

Sauti ya Buhimila Shala Mwenyekiti wa Utamaduni Mkoa wa Simiyu

Tamasha la Utamaduni Kanda ya Ziwa limezinduliwa rasmi katika Viwanja vya ccm wilayani Bariadi tarehe 05. 07. 2024 na litakuwepo kwa Muda wa Siku tatu ambapo kilele chake ni Tarehe 07. 07. 2024