Maswa:Ni matusi kuwaita watoto majina ya ujombani
3 June 2024, 5:34 pm
“Migogoro ya ndoa na mipalanganyiko yakimahusiano imeendelea kuwa na athari kwa malezi na makuzi ya mtoto nchini hali inayopelekea watoto wengi kukosa haki zao za msingi.”
Na,Daniel Manyanga
Wanawake na mabinti wametakiwa kuwaita watoto wao majina halisi ya baba zao nakuacha tabia yakuwabadilishia watoto hao ubini wa majina ya baba zao halisi na kuwaita majina ya upande wa mwanamke kutokana na hali za kimaisha kuwa nzuri.
Hayo yamesemwa na mkaguzi msaidizi wa jeshi la polisi wilayani Maswa mkoani Simiyu , Magreth Mwinuka ambae pia ni mkuu wa dawati la jinsia wilayani hapa wakati akitoa elimu ya malezi na makuzi pamoja na haki za mtoto kwa wananchi kupitia Sibuka fm.
Afande Mwinuka ameongeza kuwa wanawake wengi wamekuwa sehemu ya migogoro kwenye mahusiano ya ndoa kwa kushindwa kuwa wakweli pindi wanapokuwa wajawazito hivyo kushindwa kumtambua baba halisi wa mtoto na kuanza kuwabambikizia watu wengine kwa kuangalia hali za kimaisha zao ili kupata unafuu wa malezi na makuzi kwa mtoto.
Neema Steven mkazi wa mtaa wa nguzo nane wilayani hapa akizungumza na Sibuka fm amewaasa wanawake kuwa na hofu ya Mungu nakuwalea watoto kwa kuzingatia misingi bora ya kimalezi bila ya kujali hali za kimaisha za baba zao halisi.