Maswa queens na Raha queens hakuna mbabe Simiyu
6 May 2024, 5:49 pm
Utamu wa ligi ya wanawake Simiyu wafikia pazuri huku vipaji vya mpira wa miguu kwa wanawake vikiibuliwa na kupelekea wazazi na walezi wa vijana wa kike kuhamasisha mabinti zao kucheza mpira wa miguu
Na,Paul Yohana
Fainali ya kwanza ligi ya mabingwa wanawake mkoa wa Simiyu imefanyika katika uwanja wa nguzo nane maswa kati ya Maswa warriors queens ya Maswa na Raha queens ya Baraiadi na kuhushudia mchezo huo ukimalizika kwa sare ya bila kufungana
Kocha mkuu wa Maswa warriors, Shaban Kalinga amesema kuwa mwisho wa mchezo huo ndio mwanzo wa mchezo unaofuta na magoli popote yanapatikana.
Husna Salum ni timu kapteni wa Maswa warrios amekubali matokeo ya mchezo wa kwanza lakini ana imani na mechi ya marudianokuwa watafanya vizuri zaidi
Akizungumza na Sibuka sport kocha mkuu wa Raha quuens, Rajabu Komba amefurahishwa na matokeo ya bila kufungana ugenini akiwa na matumaini makubwa ya kufanya vizuri wakiwa nyumbani katika uwanja wa halmashauri ya Bariadi
Kwa upande wake kapteni wa Raha queens, Ester Mussa amewatoa hofu wapenzi na mashabiki wa mpira wa miguu mkoa wa Simiyu hasa wakazi wa Bariadi wasiwe na shaka kwani watafanya vizuri katika mchezo wa marudiano na kuibuka mabingwa mkoa.
Fainali ya pili itapigwa mei ,12/2024 katika uwanja wa halmashauri ya mji wa Bariadi ambapo mshindi ataenda kuwakilisha mkoa katika mashindano ya mabingwa wa mikoa kwa mpira wa miguu upande wa wanawake