Wanawake jamii ya kihadzabe Meatu waomba msaada wa Rais Samia
1 March 2024, 5:03 pm
Jamii ya kihadzabe inayoishi pembezoni mwa pori la hifadhi Makao Wilayani Meatu Mkoani Simiyu yahofia kutoweka kutokana na mabadiliko ya tabia ya Nchi.
Na,Alex Sayi
Wanawake wa jamii ya kihadzabe wamuomba Rais Dkt,Samia kulinusuru kabila hilo ili lisiweze kutoweka kutokana na mabadiliko ya tabia ya Nchi.
Hayo yamesemwa na kina mama jamii ya kihadzabe Bi,Weyeweye Khakhaha na Bi,Shuli Mujuli walipokuwa wakizungumza na Radio Sibuka fm.
Weyeweye ameongeza kuwa kutokana na mabadiliko hayo wanawake wa Jamii hiyo kwa sasa wanalazimika kuolewa na makabila mengine hali inayowawia ugumu kuyazoea mazingira hayo.
Kwa upande wake Bi,Shuli Mujulu amesema kuwa kwa sasa wanashindwa kupata vyakula vyao vya asili ikiwemo Matunda, Asali, Mizizi na Nyama hasa Nyama ya Nyani.