DC Maswa atahadharisha wanaotorosha mazao ya nafaka
7 February 2024, 1:56 pm
Mkuu wa Wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu Mhe Aswege Kaminyoge amewatahadharisha Wafanyabiashara wa Mazao ya Nafaka utoroshaji na kukwepa kulipa Ushuru wa Mazao hayo.
Mhe Kaminyoge amesema hayo katika kikao cha Wadau wa Kilimo na Mazao Mchanganyiko kilichofanyika Katika ukumbi wa Halmashauri hiyo.
Paul Maige ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa amesema kuwa mfumo huu wa Stakabadhi gharani ni Mzuri maana utamnufaisha Mkulima moja kwa moja na Halmashauri pia.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Chama kikuu cha Ushirika Mkoa wa Simiyu (SIMCU ) Lazaro Walwa amesema kuwa wao wamejiandaa kikamilifu kwenye zoezi hilo ambalo lina lengo la Kumkomboa Mkulima mdogo wa Maswa na Mkoa wa Simiyu.
Baadhi ya Wafanyabiashara wa Mazao mchanganyika hapa Maswa wamepaza sauti zao kwa Mkuu wa Wilaya kuhusu changamoto zilizojitokeza katika Misimu iliyopita Halmashauri wamejipangaje kwa Mfumo huu Mpya wa ununuzi wa mazao kwa njia ya Stakabadhi gharani.