Sibuka FM

Sibuka Fm: Kongole TADIO, Vikes kwa elimu ya kutangaza kidijitali

10 July 2023, 3:22 pm

Baadhi ya waandishi wa Sibuka Fm wakifuatilia mafunzo ya habari za mtandao. Picha na Nicholaus Machunda

Waandishi wa habari wa kituo cha Radio Sibuka Fm wamepatiwa mafunzo ya kuandaa na kutangaza habari za mtandao ili kuendana na kasi ya ushindani wa teknolojia, mafunzo yaliyofanyika katika ofisi za Sibuka Fm zilizopo mjini Maswa mkoani Simiyu.

Na Nicholaus Machunda

Waandishi  wa  habari  wa  kituo  cha Radio Sibuka Fm  wameishukuru Tadio  kwa kutoa elimu ya namna  ya  kutangaza  habari kwa njia ya mtandao https://radiotadio.co.tz/sibukafm

Wamesema  kuwa  kupitia  mafunzo  hayo sasa  watakuwa  na uwezo  wa  kuifikia  jamii katika  nyanja  zote  za  masafa  ya  Radio na  habari  za  kwenye  mtandao.

Sauti ya Paul Yohana na Neema Solo

Aidha waandishi  hao  wamesema  kuwa  wamejifunza namna  ya  kuweka  na kutangaza habari  kwenye mtandao  na  ikawafikia  watu  wengi  zaidi  ya  kutoka  ndani  na  nje  ya  masafa  ya  Radio   ili  kuendana  na  ulimwengu  wa  sasa  wa  teknolojia.

Sauti ya Neema na Paul waandishi wa habari Sibuka fm

Hilali  Ruhundwa  ni  mhariri  wa  Radiotadio amesema  kuwa  wameamua  kuwafuata  waandishi  kwenye  vituo  vyao  vya  Radio  ili kuwajengea  uwezo  wa  kujua  namna  ya  kutanaza  habari za  mtandao  ili  kuendana  na  kasi  ya  dunia.

kuweka  na kutangaza habari  kwenye mtandao 

Sauti ya Hilali Ruhundwa
Mhariri wa Radiotadio Hilali Ruhundwa (mwenye miwani) akitoa maelekezo kwa waandishi wa Sibuka fm

Ruhundwa  amesema  kuwa  mafunzo hayo  yameandaliwa  na  TADIO  kwa  Kushirikiana  na VIKES   yakiwa na  lengo  la  kuhakikisha  Radio  jamii  zinakuwa  na  uelewa  wa  kutangaza  habari  za  mtandao  kwani  kwa sasa  dunia  ipo  huko. 

Sauti ya Hilali Ruhundwa