WILAYA YA MASWA YAJA NA MKAKATI WA KUTAMBUA WAJAWAZITO WOTE ILI KUPUNGUZA VIFO VITOKANAVYO NA UZAZI..
1 July 2022, 4:28 pm
Wilaya ya Maswa imekuja na mkakati wa kuwa Dafutari maalumu la kuwatambua akina mama wajawazito wote kwenye maeneo wanayoishi ili kuepusha vifo vya mama wajawazito…
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mh Aswege Enock Kaminyoge wakati akitoa Elimu kwa Wananchi kupitia Radio Sibuka fm na Kusema kuwa mkakati huu wa utasaidia kupunguza vifo vitokanavyo na Uzazi….
Insert DC Maswa Aswege Kaminyoge.
Mh Kaminyoge amesema licha ya Halmashauri ya Wilaya kupokea Fedha Zaidi ya Shilingi Bilioni moja kwa mwaka wa Fedha 2020/ 2021 kwa Ajili ya kuboresha Huduma za Afya ikiwemo ujenzi wa Zahanati na Vituo vya Afya na amewataka akina mama wajawazito kwenda kijifungulia kwenye Vituo hivyo..
Insert 02. DC Maswa Aswege Kaminyoge.
Akitoa taarifa ya Wajawazito waliojifungulia kwenye vituo vya Afya Mratibu wa Huduma ya Afya ya Baba, Mama na Mtoto wilaya ya Maswa Dokta Angella Ngaiza amesema kuwa Namba ya wanaojifungulia vituoni imeongezeka hadi kufikia Asilimia 91.4 % kwa Robo ya kwanza (Januari- Marchi 2022).
Insert 03. Dr Angella Ngaiza
Dr Ngaiza amesema mafanikio hayo yanatokana na kuweka Utaratibu wa Kuwatumia Wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii kuwa na Daftari la kuwabaini wajawazito wote kwenye mtaa na Changamoto zao ili kuwasaidia mapema..
Insert 04. Dr Angella Ngaiza