TARURA Maswa Kuboresha Barabara zote za Kiuchumi
28 August 2021, 8:36 pm
Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini Wilayani Maswa Mkoani Simiyu Mhandisi David Msechu amewaomba Madiwani Kushirikiana na kamati za maendeleo za kata ili kulinda Miundo mbinu ya Barabara zinazojengwa ili zidumu zaidi..
Hayo ameyasema katika kikao cha Baraza la Madiwani baada ya kutakiwa kutoa ufafanuzi wa Mkakati wa TARURA katika kuboresha Miundombinu ya Barabara katika kuelekea msimu wa masika ambapo barabara nyingi za Vijijini zimekuwa hazipitiki.
Mhandisi Msechu amesema kuwa Madiwani washirikiane na Wenyeviti wa vitongoji katika kuwahamasisha wananchi katika kufungua Barabara ambazo hazifungulia maeneo ya vijijini na Mjini ili ziingizwe kwenye mpango wa Bajeti wa TARURA na Kuboreshwa zaidi huku akimpongeza mwenyekiti wa Kitongoji cha Nyambiti kwa kuhamasisha wananchi wake.
Kwa Upande wa Madiwa Wameishauri Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini TARURA wilaya ya Maswa kutoa kipaumbele kwa Barabara muhimu za kiuchumi ili ziweze kupika kwa Urahisi katika Kusafirisha Mazao.
Naye mwenyekiti wa Chama cha Mpainduzi wiaya ya Maswa Mhandisi Paul Jidayi amesema kuwa kata yoyote ikiwa na Migogoro na changamoto katika kuleta Maendeleo kwa wananchi aliyefeli hapo ni Diwani na hana cha kujitetea katika Chama.
Aidha Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Maswa Mh Paul Maige ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Mama Samia Suluhu Hasani kwa kuwaongezea Fedha zaidi ya Bilioni tatu zitakazoenda kuondoa changamoto ya miundombinu ya Barabara na ujenzi wa Mitaro.