Dc Maswa awashukia viongozi wazembe
23 April 2024, 6:12 pm
Wananchi wakeleka na utendaji kazi wa wenyeviti wa vitongoji na vijiji kushindwa kuwasikiliza kero zinawakabili ambazo zipo kwenye uwezo wa viongozi hao hivyo kuondoa uaminifu kwao
Na,Paul Yohana
Mkuu wa wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, Aswege Kaminyoge awewataka wenyeviti wa vitongoji na vijiji kufanya mikutano ya hadhara kwa wananchi ili kusikiliza kero na kuzitafutia ufumbuzi na siyo kusubiri viongozi wa ngazi za juu.
Aswege Kaminyoge ameyasema hayo wakati wa mkutano wa hadhara wa mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Simiyu uliofanyika katika kijiji na kata ya Lalago ambapo amesema kuwa wenyeviti wa vitongoji na vijiji wahakikishe wanafanya mikutano ya hadhara ambayo ipo kisheria ili kusikiliza kero zinazowakabili wananchi na kuona namna nzuri ya kuzitatua.
Kaminyoge amesema kuwa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ,Dkt.Samia Suluhu Hassan ametoa zaidi ya shilingi billion 10 katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta ya afya,elimu na miundombinu ya barabara.
Kaminyoge ameongeza kuwa katika swala la umeme wilaya ya Maswa imepiga hatua kubwa kwani mpaka sasa umeme umepelekwa katika vijiji vyote 120 hivyo katika bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025 watapeleka umeme kwenye vitongoji hivyo wananchi wawe na subira.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Simiyu,Shamsa Mohamed ametoa wito kwa viongozi wa serikali kuanzia ngazi ya chini hadi juu kuhakikisha wanasimamia miradi ya maendeleo inayotekelezwa kutokana na fedha zinazoletwa na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ili iweze kuleta thamani ya fedha zilizotumika na kuweza kumunufaisha wananchi moja kwa moja.