Halmashauri Kuu CCM wilaya Maswa yaridhishwa utekelezaji ilani ya chama
22 May 2023, 12:30 pm
Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Maswa imeridhishwa na utekelezaji wa ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025.
Akitoa taarifa kwa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, mkuu wa wilaya ya Maswa Mhe, Aswege Kaminyoge amesema kuwa katika kutekeleza ilani ya CCM kwa kipindi cha Januari, 2022 hadi Decemba, 2022 wilaya ilikuwa imepokea zaidi ya shilingi bilioni 30 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
Sauti ya DC Maswa Aswege Kaminyoge
Mkuu wa wilaya huyo amesema kuwa katika utekelezaji wa ilani ya CCM ya 2020/2025 katika kipindi cha Januari hadi Disemba 2022 wilaya ya Maswa imefanikiwa kuongeza zahanati, vituo vya afya na huduma zingine ikilinganishwa na kipindi cha nyuma.
Sauti ya DC Maswa Aswege Kaminyoge
Kwa upande wa Kamati ya Siasa ya wilaya iliyotembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imetoa mapendekezo na ushauri juu ya miradi hiyo ili iweze kuleta tija kwa wananchi.
Sauti ya Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya
Mayunga George ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya amesema kuwa ni vema viongozi wa CCM ngazi ya matawi na kata wakasikiliza kero za wananchi na kuziwasilisha serikalini ili zitafutiwe ufumbuzi .
Sauti ya Mayunga George- Mjumbe wa Halmashauri Kuu
Aidha Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Maswa imempongeza Rais na mwenyekiti wa CCM taifa Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoifanya katika taifa na wilaya ya Maswa kwa kuleta fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Sauti ya Mathias Shitagisha Katibu wa CCM -Maswa
Hapa chini ni picha za matukio ya Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Maswa