Maswa:RUWASA Wananchi tumieni maji yanayotoka kwenye vyanzo vilivyoboreshwa.
13 April 2023, 4:23 pm
Na,Alex.F.Sayi
Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini Wilayani Maswa Mkoani Simiyu (RUWASA)imewaasa wakazi Wilayani hapa kutumia Maji kwenye vyanzo vilivyoboreshwa ili kuepuka magonjwa ya mlipuko.
Akizungumza na Sibuka fm, Meneja wa RUWASA Wilayani Maswa Mhandisi Lucas Madaha amesema kuwa Ruwasa imeboresha huduma ya upatikanaji wa Maji kwa asilimia 74.6% ikiwa ni ongezeko la asilimia 5.8% ndani ya miaka miwili, lengo likiwa ni kufikia asilimia 85% ifikapo 2025.
Madaha ,ameongeza kuwa kwa sasa wanahudumia wakazi wapatao 255,639 wanao pata huduma ya Maji Safi na Salama kati ya wakazi 356,566 kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022,huku kiasi cha zaidi ya Sh.Billioni 5.3 kikitumika kuboresha huduma hiyo ndani ya miaka miwili.
“Kwa sasa tunatekeleza Miradi ya zaidi ya Sh.Bil 5.3,na fedha hizi tumepokea toka vyanzo tofauti kuna zaidi ya Sh,Bil3.3 toka (PforR),zaidi ya Sh.Mil 547.1 toka (PbR),Sh.Bil 1 za Covid 19,zaidi ya Sh,Mil 378.5 toka National Water Fund(NWF)na Sh.Mil 45.097 za (OC) kwa ajili ya kutekeza Miradi Maji Vijijini.”Amesema Madaha.
Madaha ameongeza kuwa RUWASA kwa sasa wanatekeleza Miradi ya Maji yenye zaidi ya Sh.Bil,2.6 Vijiji vya Malekano-Kadoto kwa asilimia (82%),upanuzi wa Mradi Seng’wa-Mandela kwa asilimia(87%),Mradi wa Maji Zabazaba kwa asilimia (45),na Uchimbaji wa Visima vipya (10) kwenye Vijiji (12),ukarabati wa Visima(30)na ufungaji wa Pamp za Mikono(23).
“Mbali na Miradi hiyo Miradi ya Maji yenye zaidi ya Sh.Bil.1.8 imekamirika na inahudumia wakazi(24,984)katika Vijiji vya Sulu,Inenwa-Kizungu,Isanga,Masela-Gumali,na Gongwa-Kidema hivyo kufanya jumla ya Sh.Bil5.3 kwa Miradi iliyokamilika na inayoendelea kutekelezwa”Amesema Mhandisi Madaha.
Akizungumzia hali ya upatikanaji wa Maji Diwani wa Kata ya G’wigwa Steven Dwese amesema kuwa kata yake yenye wakazi zaidi ya elfu kumi, Vijiji (4),Vitongoji(20)kaya zaidi ya 1600 inategemea kisima kimoja tu kwa sasa,hivyo kufanya wakazi hao kutembea umbali mrefu kupata huduma ya Maji.
“Hali ya upatikanaji wa Maji Katani kwangu bado ni tatizo wakazi wengi hawapati huduma ya Maji Safi na Salama hivyo tunaiomba Ruwasa ione umuhimu wa kusogeza huduma hiyo karibu na wananchi tunatambua mwongozo unataka mwananchi apate maji ndani ya mita (600)”Amesema Dwese.
Aidha Ellen Mwandu mkazi wa Kijiji cha Mwabayanda Kata ya G’wigwa Wilayani hapa amesema kuwa hali ya upatikanaji wa Maji kijijini hapo niyashida hasa wakati wa kiangazi kwani familia nyingi hulazimika kufuata Maji umbali mrefu kwenye vyanzo visivyo rasimi.
“kiukweli hali ya Maji hapa Kijijini ni mbaya angalau kwa sasa Mvua zinanyesha zimetusaidia hatuna shida sana hata kama Maji tunayochota sio salama sana lakini ni boro tunapata Maji yakutumia maana tunachota tu kwenye Madibwi yaliyojitenga na kwenye Mito.”Amesema Mwandu.