Kitulo FM

Makete waungana kuboresha miundombinu ya barabara

April 11, 2026, 1:38 pm

Mwenyekiti wa mji mdogo ndg joseph akitoa maelekezo kwa wananchi

Wakati mvua zikiendelea kunyesha katika maeneo mbali mbali na miundombinu ya barabara kuathirika kwa kiasi kikubwa wananchi kwa kushirikiana na viongozi wa serikali za mitaa wamekuwa mstari wa mbele katika kufanikisha changmoto hiyo inatatuliwa”.

Na, Rose Njinile

Kutokana na mvua nyingi zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbali mbali hapa nchini ikiwemo Makete, wananchi wamesisitizwa kuacha tabia ya kuwalaumu viongozi kutokana na miundombinu ya barabara kuharibika

Wananchi wakiendelea na kazi ya kufukia mashimo kwenye barabara

Hayo yamesemwa hii leo april 11,2026 na mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo wa iwawa ndg Joseph Mbilinyi  alipokuwa akizungumza na wananchi wa mtaa wa mwongolo walipokusanyika kwa pamoja  ili kufukia mashimo katika barabara ya mwongolo kuelekea ivalalila huku  akisisitiza wananchi kuwa serikali bado inaendelea na jitihada za kuhakikisha barabara zilizoathirika na mvua zinaboreshwa

Sauti ya mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo wa iwawa Joseph Mbilinyi
Mwenyekiti wa mji mdogo wa iwawa joseph akiongoza zoezi la ufukiaji wa mashimo kwenye barabara

Kutokana na umuhimu wa barabara hiyo ndg Joseph Mbilinyi amesema kuwa serikali itaendelea kufanya maboresho katika barabara hizo ambazo zimekuwa  zikiwaletea adha watumiaji wa barabara hiyo na kuwataka wawe wavumilivu na kutokuchoka kufanya maendeleo katika maeneo yao huku serikali ikiendelea kufanya jitihada za kuendelea kuboresha barabara hizo

Sauti ya Joseph Mbilinyi

Licha ya mwitikio mdogo wa wananchi katika shughuli za maendeleo,mwenyekiti wa mtaa wa mwongolo ndg Haroun Sanga amewasisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi katika shughuli hizo ambazo zinakuwa zinafanyika kwa manufaa ya wananchi wote huku akiwapongeza wananchi waliojitokeza kwenye shughuli hiyo ya kufukia mashimo kwenye barabara ili iweze kupitika kwa urahisi

Sauti ya mwenyekiti wa mtaa Mwongolo Harouni Sanga

Akizungumza kwa niaba ya wananchi waliojitokeza kwenye shughuli hiyo ya maendeleo bi Kevina Chaula ameshukuru kwa kazi kubwa iliyofanyika ya kufukia mashimo yaliyokuwa katika barabara hiyo jambo ambalo awali walikuwa wakipata adha kubwa ya kupita katika eneo hilo hasa wakati huu wa mvua  zinazoendelea kunyesha.

Sauti ya mwananchi kevina chaula