Kitulo FM

Zaidi ya bilioni 7 kutekeleza shughuli za maendeleo Makete

May 3, 2024, 8:46 am

Mh.Fransic Chaula akisoma utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi.picha na Aldo Sanga

katika utekelzaji wa ilani ya chama cha mapinduzi CCM zaidi ya bilioni saba zimetolewa na Serikali katika kata ya Iwawa ili kutekelez miradi ya maendeleo katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na Afya,barabda,umeme pamoja na Elimu.

Na Aldo Sanga

Zaidi ya Shilingi Bilioni saba zimetolewa na serikali kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2020-2024 kata ya Iwawa wilayani Makete Mkoani Njombe kutekeleza miradi mbalimbali.

Taarifa hiyo imesemwa Mei 2, 2024 na Diwani wa kata ya Iwawa Francis Chaula katika kikao cha kuelezea utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kata ya Iwawa ambapo amegusia miradi mbalimbali iliyotekelezwa katika sekta tofauti tofauti

Daniel Okoka MNEC Mkoa wa Njombe amesema alichokifanya Diwani wa kata ya Iwawa bw.Chaula ni takwa la chama kuhakikisha kila kiongozi wa kuchaguliwa anatakiwa kusoma utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi kwa wanachama na wananchi.

Abrahamu Okoka Mjumbe wa halmashauri kuu Taifa MNEC akizungumza kwenye kikao cha usomaji wa utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Na Aldo Sanga.

Naye Katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Makete Daniel Muhanza amewataka Madiwani wa wilaya ya Makete kuendelea kuandaa taarifa ya utekelezaji wa Ilani na kusoma utekelezaji wake ili chama kisiadhibiwe kwenye sanduku la kura.

katibu wa CCM wilaya Makete Daniel Muhanza akizungumza na Wajumbe

Taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya ccm kata ya Iwawa imegusa sekta ya Elimu,Afya,maji,miundombinu ya barabara,mifugo ,ardhi na maendeleo ya

baadhi ya wajumbe wakiwa katika kikao