Kitulo FM

Sekondari Mang’oto yatakiwa kutunza mazingira

May 3, 2024, 7:08 am

Shamba la miti iliyopandwa msimu uliopita Picha na Shafii

DC Sweda atembelea miradi ya maendeleo kukagua maendeleo ya miradi hiyo huku akiwataka wanaosimamia miradi hiyo kuhahikisha wanaitunza ili kuleta tija na ufanisi .

Na Shafi.

Mkuu wa Wilaya ya Makete mhe. Juma Sweda amemtaka mwalimu mkuu wa shule ya sekondari mang’oto kuwa makini kwenye kutunza mazingira na kutunza miti ambayo inepandwa kwaajili ya kutunza mazingira.

baadhi ya viongozi na wataalam kutoka halmashauri ya Wilaya ya Makete wakiwa eneo la mradi ya upandajinmiti mang’oto

Ameyasema hayo Leo tareh 2 may , 2024 katika ukaguzi wa miradi ya upandaji wa miti ya matunda kwenye shule ya mang’oto na kukagua msitu wa kanisa la Romani ulioko katika kijiji cha kisinga kata ya lupalilo kwaajili ya mwenge.

Aidha Mhe. Sweda amesema mwenge wa Uhuru utafanya uzinduzi wa upandaji wa miti ya matunda kwaajili ya kutunza mazingira na lishe mashureni ilivkusaidia kuondoa swala la udumavu katika Wilaya ya Makete

Nae Herman Mmelo afisa Misitu wa kampuni ya panda miti Kibiashara Wilaya ya Makete Amesema kunafaida kubwa Sana ya kupanda miti katika mazingira Mana inawasaidia wananchi katika kujipatia kipato binafsi, kutumika Kama kivutio Cha utalii kwenye jamii na kutunza mazingira katika Wilaya ya Makete.

Bi Pendo Mgaya amesema Kuna haja kubwa ya kuendelea kuzindua miradi hii ambayo inasaidia katika kutunza mazingira pamoja na kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ili kuendelea kutunza mazingira.