Kitulo FM

Wazabuni Makete watakiwa kusambaza vifaa kwa wakati

May 3, 2024, 7:30 am

Mwonekano wa majengo ya shule ya Sekondari Mount Chafukwe iliyopo Kata ya Mfumbi.picha na Shafii Ngole.

Kufatia kusuasua ujenzi wa baadhi ya miradi ya maedeleo inayoendelea katika wilaya ya Makete, DC Samweli Sweda amewataka wazabuni kupeleka vifaa kwa wakati ili kuendana na kasi ya ukamilishaji wa miradi hiyo kwa wakati ili kufikia malango yaliyotarajiwa

Na Shafii Ngole.

Mkuu wa Wilaya ya Makete Mh.Juma Samweli Sweda amewataka wadhabuni Wana chukua tenda katika miradi mbali mbali kusambaza vifaa kwa wakati ili kukamilisha miradi hiyo kwa dhumuni la kuanza kutumika na kuwasaidia wananchi.

Ameyasema hayo 2 May 2024 wakati timu ya uratibu wa Mwenge wa Uhuru Wilaya ya Makete ikikagua miradi ya ujenzi wa Madarasa ya kidato Cha 5 na 6 shule ya sekondari Mount Chafukwe iliyopo kata ya Mfumbi ulio gharimu kiasi cha Shillingi milioni 339 na Kituo Cha afya Cha Kata ya Mfumbi kilicho gharimu kiasi cha Shiling Milioni 120 jengo la mama na mtoto na jengo la OPD yaliyogharimu kiasi cha shillingi milioni 166 na lakin moja.

Aidha Mhe. Sweda ameitaka ofisi ya mipango kuhakikisha wanaongeza majengo mawili ya Maabala pamoja na chumba cha upasuaji kwa ajili ya kukamilisha kituo cha afya kata ya Mfumbi kwaajili ya kuwahudimia wananchi.

DC Sweda akikagua moja ya majengo

Kaimu mhandisi wa Wilaya ya Makete Ndg. Edward Nyalaja amesema ujenzi wa madarasa ya kidato Cha 5 na 6 katika shule ya sekondari Mount Chafukwe imefikia asilimia 84 wakati upande wa ujenzi na Kituo cha afya umefikia asilimia 90 ambapo wanategemea hivi karibuni miradi hiyo itakamilika.

Nae mtendaji wa kata Mfumbi Bi. Rahabu Kibona Amesema miradi itakua chachu kubwa ya maendeleo katika kata ya Mfumbi kwakuwa itakua inaongeza idadi ya huduma za kijamii katika kata hiyo.

Mkuu wa shule wa Mount Chafukwe Mwl. Ntuta Sambwe amesema mradi huo wa ujenzi wa Madarasa ya kidato Cha 5 na 6 utawasaidia watoto wengi wa Mfumbi na nje kupata elimu ambayo itawasaidia katika kuitengeneza kesho yao iliyo kuwa bora zaidi.

Baadhi ya wataalamu walioambatana na Dc Sweda katika ziara hiyo