Kitulo FM

Bodaboda Makete washauriwa kuripoti matukio ya uhalifu

May 3, 2024, 6:53 am

Picha ikionyesha kikundi cha vijana wa bodaboda kata ya Matamba wilayani Makete

Kutokana na kundi kubwa la waendesha vyombo vya moto hususani pikipiki maarufu kama bodaboda kutumia vyombo hivyo bila leseni mkuu wa wilaya ya Makete mh.Samweli Sweda ametoa rai kwa vijana hao kumiliki leseni na kutoa taarifa za matukio ya uharifu.

Na Shafii

Mkuu wa Wilaya ya Makete mhe. Juma Sweda amewaaasa wanakikundi wa boda boda na kilimo kuzingatia umakini wa kutoa taarifa mapema pale ambapo wanapata shida ili kupata usaidizi kwa haraka zaidi.

Dc Sweda aliye valia kofia yenye bendela ya Taifa Akikabidhi pikipiki kwa vijana Picha na Shafii.

Ameyasema hayo Leo tarehe 2 May, 2024 katika ukaguzi wa kikundi Cha boda boda na kilimo kilichopo kata ya Matamba Kijiji Cha mpangala ambacho kilipata mkopo wa serikali wa sh million 52.

Aidha Mhe. Sweda amewataka wanakikundi hawa kuwa na reseni ambazo zitawasaidia katika kazi zao za usafirisha na kuzingatia matumizi sahihi ya barabara

Nae afisa maendeleo ya jamii katika Wilaya ya Makete Bi. Esther Ramosai amesema dhumuni la kikundi iki ni kupunguza idadi ya vijana ambao hawana ajira mtaani na kuinua maisha ya mtu mmoja mmoja katika jamii

Theresia Lameck Mtendaji wa kata ya Matamba amesema kikundi iki kimewasaidia vijana wengi kujipatia ajira ambayo inawasaidia katika jukumu la kimaisha pamoja na kuendelea kuongeza nguvu kazi katika kata kwa kulima mazao mbali mbali.

Nae Mwenyekiti wa chama Cha boda boda na kilimo ndg. Malani Nyambo amesema kikundi iki kinawasaidia katika swala kujikimu kimaisha kwasababu wanajipatia kipato kupitia miradi inayo endeshwa na kikundi iki.

wanakikundi wakizungumza na Dc Sweda kata ya Matamba