Wahitimu tisa (9) darasa la saba watunukiwa vyeti St.Johakim pri & primal school
September 16, 2023, 6:17 pm
ikiwa ni muda mfupi baaya kumaliza mitihani ya Taifa Darasa la saba juma la wahitim tisa wametunukiwa vyeti vya kuhitim katika shule ya st,Johakim pri & Primaly school shule inayomilikiwa na kanisa katoliki parokia ya Makete Jimbo la Njombe,
na Aldo Sanga
Jumla ya wahitimu tisa (9) darasa la saba katika shule ya St.Johakim pri & primal school wametunukiwa vyeti vya kuhitimu baada ya kumaliza muda wao wa masomo katika ngazi ya Elimu ya Msingi mwaka wa masomo 2023 Iwawa Makete.
Akitoa taarifa ya shule hiyo mkurugenzi wa shule Padre,kayombo ameeleza baadhi ya mafanikio waliyo yapata tangu kuaanzishwa kwa shule ikiwa ni pamoja na taaluma ambapo amesema kwa mitihani ya kujipima shule hiyo imekua nafasi nya kwanza na kwa ufaulu wa (A) kwa ngazi ya (W) huku shule hiyo ikifanya vizuri kwa mitihani ya kujipima kwa ngazi ya mkoa,
Aidha ameongeza kua ufaulu unategemea ushirikiano wa wazazi na walimu pamoja na juhudi za mwanafunzi awapo shule,
Kwa upande wao wanafunzi walio hitim leo shule hapo wamewashukuru walimu pamoj na uongozi mzima wa shule kwa ushirikiano walio wapa hususani katika masomo yao na kuahidi kua watafanya vizuri katika matokeo ya mitihani ya Taifa.
Katika mahafar ya 13 shule ya St.Johakim Makete zaid ya kiasi cha Tsh:600,000/= kimetolewa na Falomeo Mahenge ambaye ndiye aliyekua Mgeni rasmi kwaajili ya kutatua changamoto ya nishati ya umeme kwa upande wa betri,
Bw,Mahenge ametoa pongezi kwa uongozi wa shule hiyo kwa uwekezaji waliofanya katika wilaya ya Makete kwa kusema imekua shule ya kwanza kuanzishwa katika mji wa Makete na kuanza kutoa taswila ya Elimu kwa Mfumo wa ufundishaji kwa Lugha ya Kiingeleza.