Kitulo FM

Maambukizi ya virusi vya UKIMWI Njombe sasa yafikia asilimia 10.4

November 1, 2023, 11:02 am

Makamu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Philipo Mpango akisalimiana na wananchi wa Tandala Makete baada ya mkuatano kumalizika. Picha Rose njinile

Moja ya njia mojawapo Ssrikali inaendelea kupambana ni kuhakikisha elimu inaendelea kutolewa kwa wananchi wake kuhakikisha wanajikinga na kuwalinda wengine dhidi ya maambuki ya ukimwi.

Na Rose Njinile.

Kutokana na maambukizi ya virusi vya ukimwi kuendelea mpaka kufikia asilimia 10.4 hususani mkoa wa Njombe, wito umetolewa kwa kila mwananchi kuhakikisha anajilinda na kuwalinda wengine dhidi ya maambukizi hayo.

Hayo yamesemwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipokuwa akizungumza na wananchi katika viwanja vya Diakonia Tandala. Amesema kuwa serikali inaendelea na jitihada za kupambana na maambuzi ya Virusi Vya Ukimwi.

Sauti ya makamu wa rais mh Dkt. Mpango

Aidha Dkt. Mpango amewataka viongozi wa dini, viongozi wa siasa na viongozi wa kimila kuendelea kuikumbusha jamii kuhusu kuendelea kujikinga na kujilinda na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.

Sauti ya makamu wa rais mh dkt Philipo Mpango