Wasichana 8,035 kupata chanjo ya saratani ya malango wa kizazi Makete
April 23, 2024, 10:25 pm
kupitia kampeni ya Kitafa ya chanjo ya HPV kwa wasichana wa umri miaka
Jumla wa wasichana 8035 wa umri wa kuanzia miaka 9-14 wanatarajia kupata chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi ,zoezi ambalo litafanyika kwa siku tano kuanzia April 22 hadi April 26, 2024
Akizungumza na Kitulo FM Aprili 23, 2024 mratibu wa chanjo wilaya ya Makete Ndg Huruma Mkiramweni amesema wilaya ya Makete zoezi la utoaji wa chanjo limezinduliwa katika kata Kigulu likiwa limewalenga wasichana kwa ajili ya kuwakinga na saratani ya mlango wa kizazi
Ndg Huruma Amesema chanjo hii itatolewa katika shule za msingi, shule za sekondari na maeneo ambayo wanapatikana watoto wenye umri huo hivyo wazazi na walezi wahakikishe watoto wao wanapata chanjo hii muhimu kwani saratani ya mlango wa kizazi imewalenga wanawake tu
Ikumbukwe zoezi hili la utoaji wa chanjo linafanyika nchi nzima na kwa Tanzania ilianza kutolewa mwaka 2014 na ilikua inatolewa kwa mabinti wenye miaka 14 , lakini kwa kuzingatia umuhimu wachanjo hii ya saratani ya mlango wa kizazi kwa mwaka huu inatoa kutoa chanjo kuanzia miaka 9-14 na mwaka ujao kwa maana 2025 chanjo hii itaanza kutolewa kwa mabinti wenye miaka 9