Kitulo FM

Wafugaji wa nyuki washauriwa kutumia wataalam

April 22, 2024, 12:21 pm

picha ya nyuki kwa hisani ya mtandao.

Kutokana na wafugaji wengi wa nyuki kufuga kienyeji na kutopata faida ofisi ya misitu Halmashauri ya wilaya ya Makete wameshauri wafugaji kutumia ushauri wa wataalamu ili wafuge kwa tija.

Na Bensoni Kyando.

Wananchi Wilayani Makete Mkoani Njombe wanaojishuhulisha na shughuli za ufugaji wa nyuki na ukulima wa miti wametakiwa kuwatumia wataalamu waliopo katika halmashauri ya Makete katika kushaurina namna bora ya ufugaji wa nyuki na ukulima wa miti ili waweze kupata faida kubwa kutokana kazi zao hizo.
Hayo yamesemwa na afisa misitu kutoka halmashauri ya wilaya ya Makete Ndugu Naferi Lulesu waakati wa mafunzo ya maandiko ya kuomba fedha za ruzuku kutoka mfuko wa misitu Tanzania kwa vikundi mbalimbali vya ufugaji wa nyuki na wakulima wa miti ambayo yamefanyika katika ukumbi mdogo wa halmashauri wilaya Makete .

sauti ya afisa misitu wilaya ya Makete ndugu,Nafeli Lulesu

Kwaupande mwingine Ndugu Naferi Lulesu amewataka wananchi kuendelea na ufugaji wa nyuki kwani kwahivisasa soko la asali ni lauhakika huku akiseama kuwa hata hali ya hewa inaruhusu ugugaji wa nyuki kwani kunamimea mingi ambayo ni rafika kwa nyuki wakati wa utengenezaji wa asali

sauti ya afisa misitu wilaya ya Makete ndugu,Nafeli Lulesu

Afisa mazingira kutoka halmashauri Wilaya ya Makete Bi. Upendo Mgaya amewashukuru wafugaji hao wa nyuki na waakulima wa miti kufika katika mafunzo hayo huku akisema kuwa ufugaji wa nyuki na kilimo cha miti ni mojawapo ya njia ya utunzaji wa mazingira lakini pia shughuli hizo zinawapatia wanachi kipato kinachowasaidia kuinua uchumi wao

sauti ya afisa mazingira wilaya ya Makete Bi,Upendo Mgaya

Baadhi ya wakulima hao wa miti na wafugaji wa nyuki kutoka halmashauri ya wilaya ya Makeke wamesema kuwa mafunzo yatawasaidia kwenda kufuga kitaalamu kwani kabla ya mafunzo hayo wengi wao walikuwa wafuga nyuki bila utaalamu na wanaamini kuwa kwasasa ufugaji wao utakuwa na tija kubwa

sauti za wananchi walioshriki mafunzo ya ufugaji wa nyuki.

Mafunzo hayo kwa vikundi vya wafugaji wa nyuki na wakuliama wa miti yamewezeshwa na doctor Tully Msuya kutoka makao makuu Dodoma ambaye ni mratibu wa mfuko wa misitu hapa nchini Tanzania