ukaguzi wa miradi umefanyika na kamati ya fedha Makete
April 18, 2024, 11:10 pm
katika kutekeleza miradi ya maendeleo Makete katika sekta mbalimbali kamati ya Fedha utawala na mipango imefanya ukaguzi wa miradi kwalengo la kusukuma kasi ya miradi ikamilike kwa wakati
Na Aldo Sanga.
Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango, leo April i,18, 2024, imefanya ukaguzi wa Miradi ya kimaendeleo katika Kata Mbili za Tandala na Ukwama, ili kujionea utekelezaji wa miradi hiyo sambamba na kusikiliza changamoto na utatuzi wake.
Akizungumza mara baada ya Ukaguzi wa Miradi hiyo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Mhe. Christopher Fungo, amesema kuwa, baadhi ya Miradi imechelewa kukamilika kwa wakati kutokana na changamoto ya miundombinu ya barabara kutopitika wakati wa kipindi cha mvua.
Sambamba na hayo, Mhe. Fungo, amewataka wananchi wote, ambao miradi ipo kwenye maeneo yao, wahakikishe kuwa wanashiriki kikamilifu, pamoja na kuitunza vizuri kwakuwa imekuwa ikitumia Fedha nyingi Hadi kukamilika kwake.
Kwa Upende wake, Diwani wa Kata ya Mlondwe, Mhe. Alfonse Salim, amewataka wakazi wa Kata za Tandala na Ukwama, kuiunga mkono Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika utekelezaji wa miradi hiyo, kwakuwa itakuwa na tija katika ukuaji wa uchumi kwenye maeneo yao.
Ikumbukwe kuwa, Kamati hiyo ya Fedha, Mipango na Utawala, imefanya ukaguzi wa Ujenzi wa Zahanati Kijiji Cha Ikonda, Ujenzi wa matundu ya vyoo katika Shule ya Msingi Ikonda, Ujenzi wa nyumba ya watumishi, mbili Kwa moja katika Zahanati ya Masisiwe, Ujenzi wa madarasa 15, matundu ya vyoo 20, pamoja na bwalo katika Shule ya Sekondari Lupalilo, ambapo miradi yote inagharimu zaidi ya milioni 860, za kitanzania.