Maafisa ugani watakiwa kusimamia zao la ngano Makete
April 17, 2024, 6:24 am
katika kusimamia na kutekeleza kwa vitendo mpango wa Serikali wa kufungua fulsa za kiuchumi katika Wilaya ya Makete maafisa ugani wametakiwa kusimamia kilimo cha zao la ngano kwalengo la kuleta tija kiuchumi kwa wananchi wa Wilaya ya Makete.
Na Aldo Sanga
Mkuu wa wilaya ya makete Mh:Juma Sweda amewataka maafisa ugani kusimamia ipasavyo utekelazaji wa kilimo cha zao la ngano ili kufikia malengo na kuleta tija kwa wananchi wa makete katika kuinua uchumi.
Mh:Juma Sweda amewaagiza maafisa ugani kusimamia wakulima wote waliochukua mbegu ya ngano kwaajili ya kupanda huku akiwataka kutoa taarifa ya maendeleo ya zao hilo kila wakati ili kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza wakati wa ukuaji wa ngano.
Itakumbukwa kuwa Serikali imetoa jumla ya tani 500 za ngano ikiwa na lango la kufanya zao hilo kuwa nizao la kimkakati lililolenga kumwinua mwananchi wa Makete kiuchumi na kua wazalishaji wa ngano katika taifa la Tanzani .
Kwa upandewake mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Makete Williamu Makufwe amewataka maafisa ugani kuwa watatuzi wa changamoto za wakulima badala ya kuibua changamoto zisizo na tija kwa manuufaa ya wakulima na wanamakete kwa ujumla.
Baadhi ya maafisa ugani wameeleza baadhi ya changomoto zinazowakabili kuwa nipamoja na ,wakulima kutokuwa na mitaji,kilimo cha mazoeya,bei ya soko kuwa chini,mfumo wa malipo ambapo kwasasa mnunuzi anatumia mfumo wa malipo yasiyo ya keshi jambo ambalo limekua na mwitikio hasi kwa wakulima.
kwa upande wa bodi na nafaka na mazao mchanganyiko CPB wameeleza umuhimu wa zao la ngano na jinsi litakavoweza kuwainua wananchi wa Makete huku wakijipanga juu ya kuhakiki ubora wa zao hilo ili kukidhi soko la dunia.