Tatizo la maji Makete latafutiwa muarobahini.
March 26, 2024, 5:17 pm
ikiwa serkali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imejikita katika kumtua mama ndoo kichwani wilaya ya Makete imefika zaidi ya 91%katika utekelezaji wa mkakati huo ,
Mkuu wa Wilaya ya Makete ambaye pia ni mgeni rasmi wa kikao Cha wadau wa maji Wilaya ya Makete Mhe. Juma Sweda amesema kuwa serikali ya awamu ya sita imetekeleza miradi mingi katika kipindi hiki asa katika swala Zima la miundombinu ya maji ambalo linaelekea kupungua kwa asilimia 91.6 katika Wilaya ya Makete.
Ameyasema hayo Leo tarehe 25 Machi, 2024 katika kikao Cha wadau wa maji Wilaya ya Makete kilicho fanyika ukumbi wa Almashauri ya Wilaya ya Makete.
Aidha Mhe. Sweda anewashukuru wananchi kwa kutunza vyanzo vya vinavyo patikana katika Wilaya ya Makete.
Nae afisa maendeleo ya jamii Mkoa wa Njombe Ndg. Seleman mdaba amesema kwamba Mkoa una mpango kazi ambao unaandaliwa kwaajili ya kuwafnya wakazi wote kufikiwa na maji kwa Bei nafuu.
Meneja wa wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini(RUWASA)mwandishi Innocent Lyamuya amesema ili kufanikisha malengo yalio kusudiwa na serikali ya uanzishwaji wa RUWASA na Vyombo vya utohaji huduma ya maji ngazi ya jamii ni lazima kushirikisha mamlaka nyingne za serikali na RUWASA, watendaji wa kata na vijiji kushirikiana na CBWSOs kuwahimiza wananchi kutoa Ankara za maji na viongozi wa Vyombo vya utohadi huduma ya maji kuhusishwa katika vikao vya kamati za maendeleo ya Kata (KAMAKA) ili kuendeleza kutunza miradi ya maji.
Nae mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya Makete Mhe. Christopher Fungo amewataka viongozi wa kata kushirikiana na watendaji wa mamlaka ndogo za maji katika kata ili kutunza na kusimamia vyanzo vya Mana na ukusanyaji wa Ankara za maji kwa ufasha kwa dhumuni la kuendeleza miradi ya maji