DC Makete aiagiza MAKEUWASA kuhakikisha mradi wa maji Isaplano unakamilika
February 6, 2024, 9:24 pm
Ikiwa ni muda mrefu umepita tangu kuanza kutekelezwa kwa Mradi wa Maji katika kata ya Isaplano Mkuu wa wilaya ya Makete Mh.Juma Samweli Sweda ameagiza Mamlaka ya Maji safi na Mazingira kuhakikisha mradi huo unakamailika kwa wakati
Na Ombeni Mgongolwa
Mamlaka ya Maji Safi na Usafi mazingira Makete Mjini (MAKEUWASA), imetakiwa kushirikiana na Mamlaka ya Maji Mkoani Njombe, (NJUWASA) katika kuhakikisha wanakamilisha mradi wa Maji kutoka Kata ya Isapulano hadi Maleutsi ili kuwaepusha wananchi na adha ya upatikanaji wa huduma hiyo muhimu.
Mkuu wa Wilaya ya Makete Mhe. Juma Sweda amesema hayo leo Februali 6, 2024 wakati wa ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maende
Mhe. Sweda amesema kuwa kukamilika kwa mradi huo kutawasaidia wananchi wa maeneo hayo kupata huduma ya maji kwa urahisi kutokana na umuhimu wake katika maisha ya kila siku.
Aidha amewataka wananchi wanaoishi katika Kata hizo, kutunza vyanzo vya maji, ikiwa ni pamoja na kutofanya shughuli mbalimbali za kibinadamu katika maeneo hayo, kama vile ufanyaji kilimo pamoja na ukataji wa miti hovyo, sambamaba na kupanda miti isiyo rafiki na maji.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Makete (MAKEUWASA), Bw. Alphonce Kahimba, amesema kiasi cha shilingi bilioni mbili zimetengwa ili kukamilisha mradi huo wa Isapulano-Maleutsi ikiwa ni gharama za ununuzi wa bomba na ulazaji wa bomba katika kilometa 43 pekee.
Ikumbukwe kuwa, Mkuu wa Wilaya ya Makete, Mhe. Juma Sweda, akiwa na kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya pamoja na wataalamu mbalimbali Wilayani Makete, inaendelea na ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo , ambapo kesho Februali 7, itakuwa katika Kata ya Kitulo