Wananchi wahimizwa kufuata sheria pindi matukio ya uharifu yanapojitokeza
February 1, 2024, 6:31 pm
Imeelezwa kuwa elimu ni nguzo pekee ya wananchi kuweza kutambua sheria ili kufahamu haki na wajibu wao pindi ambapo wanapokuwa na changamoto mbali mbali pamoja na kutoa ushirikiano na vyombo husika katika kufanikisha haki inatendeka pindi ambapo uharifu unapojitokeza
Na Rose Njinile
Wito umetolewa kwa wananchi wilayani Makete mkoani Njombe kuacha kujichukulia sheria mkononi pindi matukio ya kiuharifu yanapokuwa yamejitokeza katika jamii zao ili kuepuka uvunjaji wa sheria.
Hayo yamesemwa hii leo Februari Mosi 2024 kwenye maadhimisho ya siku ya sheria nchini ambayo kiwilaya yamefanyika katika ukumbi wa Madiahan Villa Makete mjini.
Katibu Tarafa, Tarafa ya lupalilo ndg Agustino Ngailo akizungumza na wananchi kwenye wiki ya sheria
Katibu Tarafa, Tarafa ya lupalilo ndg Agustino Ngailo akimuwakilisha mkuu wa wilaya ya makete mh Juma Sweda amesema kuwa kila mwananchi anawajibu wa kutambua namna bora ya kuweza kutambua sheria pindi matukio ya ukatili au uhalifu yanapotokea
Aidha ndg Ngailo amesema kuwa licha ya vitendo vya kikatili kuendelea kutokea katika jamii huku baadhi ya akina baba kufanyiwa vitendo hivyo vya kikatili wamesisitizwa kutonyamaza na badala yake watoe taarifa ili sheria ichukue mkondo wake
baadhi ya wanafunzi wa veta wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi
Hakimu mkazi mfawidhi mh Ivan Msack amewapongeza wadau Wa mahakama kwa kuendelea kushirikiana na mahakama katika utoaji haki huku maboresho yakiendelea kufanyika katika mahakama ili kuwa na miundombinu rahisi ya utoaji wa haki jinai na mwananchi aweze kupata huduma yake kwa haraka zaidi
Apolo laizer ni mwanansheria wa halmashauri ya wilaya makete kwaniaba ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ndg William Makufwe ameipongeza mahakama katika kuwahimiza wananchi kuendelea kuutumia muhimili wa mahakama kutatua au kupata masaada wa migogoro mbali mbali inayojitokeza
Mwanasheri wa Halmashauri (w)Makete Apolo laizer akizungumza na wannachi kwenye wiki ya sheria
Rosemary Wambali akisoma Hotuba mbele ya mgeni rasmi kwaniaba ya wanachama wanasheria wa kujitegemea (TLS)amewaomba wadau mbali mbali kuendelea kushirikiana na Tasisi zinazoshughulika na haki jinai ili kuweza kuhakikisha haki inapatikana kwa ustawi wa Taifa na wananchi kwa ujumla
Kwa upande wa Mwendesha mashtaka wilaya ambaye pia ni inspekta wa jeshi la polisi Benstard Wwoshe akisoma hotuba mbele ya mgeni rasmi amesema kuwa utoaji na upatikanaji wa haki inawezekana ikiwa kutakuwa na mfumo imara kama vitendea kazi vya kisasa (TEHAMA),pamoja na uwepo wa miundombinu wezeshi baina ya taasisi za haki jinai
mwendesha mashtaka wilaya Benstard Mwoshe akitoa hotuba mbele ya mgeni rasmi na wananchi
Nao baadhi ya wadau mbali mbli wakiwemo Viongozi wadini, Shiriki la mapao, Takukuru, Veta, wamewasii wananchi kuendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwenye mahakama pamoja na vyombo vinavyohusika na uchunguzi ili haki iweze kupatikana huku wakiwasisitiza kuendelea kujitokeza katika sherehe hizo ili kupata elimu inayohusu sheria
Maadhimisho hayo yamekwenda sambamba na kauli mbiu isemayo UMUHIMU WA DHANA YA HAKI KWA USTAWI WA TAIFA NAFASI YA MAHAKAMA NA WADAU KATIKA KUBORESHA MFUMO JUMUISHI WA HAKI JINAI