January 31, 2024, 7:56 am
katika mwendelezo wa ziara za jukwaa la ustawi wa jamii Makete kutoa elimu ya malezi mkurugenzi mtendaji akiambatana na baadhi ya wataalam kutoka Halmashauri wametembelea kata ya Ipepo na kutoa msaada wa vifaa vya shule kwa watoto wanaotoka ktk mazingira Magum
na Lulu Mbwaga
Jukwaa la Ustawi wa mtoto la Wilaya ya Makete leo limetembelea kata ya Ipepo kwa ajili ya kutoa elimu ya malezi kwa wototo na kuwakabidhi vifaa vya shule kwa wanafunzi wanaoishi mazingira magumu
Wanafunzi hao wamekabidhiwa vifaa mbalimbali ikiwemo madaftari, kalamu, mashati, sweta ,viatu na mavazi mengine
Akikabidhi vifaa hivyo mbele ya Kamati ya Maendeleo ya Kata (Kamaka) kata ya Ipepo Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Makete na Mwenyekiti wa Jukwaa la mtoto amesema vifaa hivyo vimetokana na michango ya wadau wa ndani ya Makete na nje ya Makete ambapo amewaomba wadau kuendelea kuchangia
Amesema lengo la jukwaa hili ni kutoa elimu na mahitaji kwa watoto ili waweze kupata elimu kwa kuwawezesha mahitaji muhimu na kuondokana na ukatili ambao unapelekea watoto kushindwa kumaliza masomo yao
Aidha amewaasa wanafunzi kusoma kwa bidii na kutumia vifaa hivyo walivokabidhiwa katika kuboresha taaluma yao kwa kufaulu vizuri darasani kwani Serikali ya awamu ya sita imeboresha na inaendelea kuboresha miundombinu ya shule
Mwalimu Thomas amesema jambo lililofanyika ni zuri na linawafundisha na kuwambusha kusaidia watoto ambao hawana mahitaji muhimu sambamba na hilo amemshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Makete kwa kuhamasisha na kuwa mstari wa mbele katika kuwakumbuka watoto
Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi waliopata mahitaji hayo Ostela Sanga ameshukuru na kuahidi kuendelea kufanya vizuri katika masomo na kupewa vifaa hivyo vimeleta hamasa zaiadi ya kusoma kwa bidii
Jukwaa la ustawi wa mtoto linaongozwa na Mkurugenzi Mtendaji halmashaur ya Wilaya ya Makete na Leo limezindua zoezi la kutoa elimu ya malezi na kugawa vifaa vya shule katika kata ya Ipepo ambapo zoezi hili litafanyika Wilaya yote ya Makete