Ded William Makufwe awataka watendaji kusimamia mapato
January 30, 2024, 9:55 pm
Kutokana na upotevu wa mapato Ded Makufwe amewataka Watendaji hususani katika maeneo yote yenye mageti kuahkikisha wanasimamia kikamilifu kudhibiti mianya yote ya utoroshaji wa mapato ambayo ndio uti wamgongo wa Halmashauri ya Makete
na Mwandishi wetu
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya Makete Ndg. William Makufwe amewaasa viongozi wa Kata ya Ipelele kuhakikisha wanazuia upotevu wa mapato ya ndani kwani bila ukusanyaji wa mapato vizuri Halmashauri haiwezi kufanikiwa kuendeleza huduma za kijamii
Amesema mapato ndio uti wa mgongo wa Halmashauri kwani kupitia mapato ya ndani Halmashauri imefanikiwa kufanya shughuli nyingi za maendeleo ikiwemo ujenzi wa kituo cha afya Mbalatse, ujenzi wa nyumba za walimu ,ujenzi wa vyumba vya madarasa na inaendele kumalizia maboma ambayo yalianzishwa kwa nguvu za wananchi
Akizungumza katika kikao cha Kamati ya Maendeleo ya kata (Kamaka) Kata ya Ipelele Mkaoni Njombe, tarehe 29/1/2024 amesema endapo viongozi wakashirikiana katika kuhakikisha wanatoa elimu na kuzia mianya ya upotevu wa mapato shughuli nyingi za Maendeleo zitafanikiwa
Makufwe amesema kuwa mkakati wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete ni kuziba mianya ya utoroshaji wa mapato na kuhakikisha wakusanyaji wa mapato wanafanya kazi kwa weledi mkubwa
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya maendeleo ya kata akiwemo Alimivu Sanga na Nelson Sanga wameahidi kushirikiana na watendaji wa vijiji katika kuzuia upotevu wa mapato huku wakioomba Serikali iweze kukarabati miundombinu ya barabara kwani itasaidia kuongeza mapato
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Makete Ndg William Makufwe anaendelea kufanya ziara katika kata mbalimbali ambapo mpaka sasa kata zaidi ya 8 amekwisha kutembea ili kusikiliza kero na kuzitatua ambapo Leo januari 30/2024 yupo kata ya Ipepo