Dc Juma Sweda Ametembelea kaya zilizoezuliwa na upepo Ipelele Makete
January 30, 2024, 9:26 pm
Tayari takribani nyumba saba zimeshajengwa ikiwa ni hatua za kunusuru kaya zilizokosa makazi baad ya mvua na upepo mkali kuezua nyumba siku za hivi karibuni katika maeneo kadha katika wilaya ya Makete ambapo serkali wadau na wananchi wamechangia nguvu zao kukamilisha makazi ya muda
na Lulu Samsoni
Mkuu wa wilaya ya Makete Mhe. Juma Sweda na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Makete Ndg. William Makufwe leo tarehe 29 Januari, 2024 wamefika shule ya Sekondari Ipelele kukagua ukarabati wa vyumba vya madarasa na nyumba za walimu ambapo tayari ukarabati umemalizika na kutembelea kaya ambazo nyumba zao ziliezuliwa bati na kubomoka wiki iliyopita
Akizungumza mara baada ya ukaguzi huo Mkuu wa Wilaya, amesema wameamua kuchukua hatua ya haraka kununua vifaa ili ukarabati madarasa hayo na nyumba za walimu zilizoezuliwa na Upepo.
Aidha amewapongeza wananchi wa Kata ya Ipelele wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya Ndg. Clement Ngajilo kwa ushirikiano mkubwa waliouonyesha huku akiwapa pole walimu kwa kukosa makazi kwa muda na amewahakikishia kesho watarejea katika nyumba zao
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya amewaagiza mafundi kukamilisha ukarabati kabla ya tarehe 31 Januari, 2024 ili masomo yaendelee kwa Wanafunzi huku akimuagiza Mkuu shule kupanda miti kuzunguka eneo lote la shule
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji Cha Mbanga Ndg. Nelson Fungo amesema wananchi na wadau wameshirikiana na kufanikiwa kuwajengea nyumba za muda wananchi 7 na kuwachangia chakula kama mahindi, ngano na maharage
Baadhi ya wananchi ambao nyumba zao ziliezuliwa akiwemo Bi. Helenida Chaula, Bhabhikie Mtepa na Betina Sanga wameushukuru Uongozi wa Halmashauri kwa kuwaona huku wakiahidi kupanda miti katika makazi yao ili kupunguza maafa yatokanayo na upepo mkali