Milioni 622 kufidia ujenzi wa barabara Makete
January 25, 2024, 8:28 am
Ikiwa tayari ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami katika eneo la ujuni umeshaanza kwa zaidi ya kilometa 3 serikali imeendelea kutoa fedha ili kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo kutoka Makete ,kupitia Nkenja kwenda Mbeya
Na Aldo Sanga
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amemuagiza Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi kutenga kiasi cha Shilingi Milioni 622 kwa ajili ya kulipa fidia kwa kaya 31 za wananchi waliopisha ujenzi wa barabara ya Ndulamo-Nkenja-Kitulo (km 42.2) inayojengwa kwa kiwango cha lami.
Ameeleza kuwa katika ujenzi wa barabara hiyo inayounganisha Mkoa wa Njombe na Mbeya, kilometa 7 tayari zimekamilika kujengwa kwa kiwango cha lami na kusisitiza kuwa ujenzi wake utakapokamilika utaleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi.
Mh. Bashungwa ameyasema hayo wakati Akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Ujuni wakati wa ukaguzi wa Ujenzi wa Barabara ya Lami unaoendelea kutoka Nkenja-Ujuni-Kitulo yenye urefu wa Km 7.5