Makete washiriki misa ya shukrani mapokezi ya askofu Eusebius Kyando
January 21, 2024, 9:53 pm
Ikiwa nisiku chache tangu Askofu Eusebius aingizwe kazini katika jimbo la Njombe mapema hii leo amefanya ziara yake ya kwanza katika parokia ya Makete ibada iliyohudhuriwa na mamia ya wanamakete wakiwemo viongozi mbalimbali wa vyama na serikali.
Na Mwandishi wetu
Askofu wa Jimbo Catholic Njombe Eusebius Kyando leo 21 Januari, 2024 ameshiriki Ibada ya Shukrani iliyofanyika Kanisa Katoliki Parokia ya Makete na kuwaomba waumini waendelee kumuombea ili kuwezesha Utumishi wake
Katika Ibada hiyo iliyofanyika leo, Mhashamu Kyando amesema katika Utumishi wake bila kumtanguliza Mungu ni sawa na kazi bure, huku akiwaomba waumini wote kumuombea kwani hakuna kazi iliyonyepesi Duniani.
Wakati huohuo, Mkuu wa Wilaya ya Makete Mhe. Juma Sweda pamoja na kutoa pongezi kwa Askofu huyo kuteuliwa kuliongoza Kanisa Katoliki Jimbo la Njombe, amesema Serikali itaendelea kufanya kazi kwa ushirikiano wa Karibu na watu wote bila kujali dini ya mtu lwa lengo la kuleta Maendeleo Wilayani Makete na Taifa kwa ujumla.
Wakati huohuo amewataka Wazazi na Walezi ambao wanawatoto wanaopaswa kuripoti shuleni wawapeleke watoto wao mara moja ili waweze kupata Elimu ambayo ni haki yao”.
Kwa upande wake Mhandisi Anthony Sanga ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi amesema anatambua kazi aliyopewa Baba Askofu huyo ni ngumu lakini wataendelea kumuombea kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu ambaye amemtuma aweze kuifanya kazi ya Uaskofu na kuahidi kuwa Serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa Makanisa yote na Wananchi wake.
Mbunge wa la Makete Mhe. Festo Sanga amempongeza Askofu Kyando kwa kuaminiwa na kuwapongeza Wadau wa Maendeleo Makete kwa kuendelea kujitoa kwa hali na Mali katika kuunga mkono jitihada za Serikali kuwaletea Maendeleo Wananchi Wilayani Makete
Askofu Eusebius Kyando ni Askofu wa tatu wa jimbo Katoliki la Njombe ambaye aliingizwa rasmi kazini