Dc Makete afanya ziara ya kushtukiza katika hospitali ya wilaya Makete
January 19, 2024, 10:34 pm
Katika mwendelezo wa ziara za Mkuu wa Wilaya ya Makete Mh. Samweli Sweda, mapema hii leo amefanya ziara ya kushtukiza katika hospitali ya wilaya ya Makete na kubaini baadhi ya changamoto ikiwemo baadhi ya vifaa tiba kutotumika tangu 2021.
Mkuu wa wilaya ya Makete Mh.Juma Samweli Sweda ameagiza idara zote zenye miradi ya maendeleo ambayo bado haija kamilika kuhakikisha inakamilika na kukabidhiwa kwa wananchi ifikapo januari 25 /2024.
maagizo hayo ameyatoa kwenye kikao cha wakuu wa idara wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete mara baada ya kukamilisha zira yake yakushitukiza katika Hospitali ya Wilaya ya Makete ambapo pamoja na hali ya ufanisi wa miradi katika idara ya afya Mh.Sweda amebaini baadhi ya changamoto ikiwemo baadhi ya vifaa tiba vilivyopo katika Hospitali ya Wilaya kutotumika
Akipokea maagizo hayo mganga mkuu wa wilaya ya Makete Dr.Ligobeth kalisa amekili kuwepo kwa baadhi ya changamoto ikiwemo badhi ya vifaa tiba kutotumika Ikiwemki baadhi ya mashine ambazo hadi sasa hazitumiki huku akieleza kua kwasasa tayari wameshaanza kusambaza vifaa tiba katika baadhi ya vituo vya afya ikiwemo kituo cha Afya Kitulo
Katika hatua nyingine Mh.Sweda ameagiza Halmashauri kuongeza juhudi katika kukusanya mapato ambapo amesema kwa takwimu za mwezi desemba Halmashauri ya Makete iko nyuma kwa ukusanyaji wa mapato kwa 15% ukilinganisha na halmashauri zingine za mkoa wa Njombe