DC Sweda aahidi laki tano matengenezo barabara Kinyika-Mlondwe
January 19, 2024, 6:30 pm
na mwandishi wetu.
Imeelezwa kuwa barabara ni moja ya njia inayowasaidia wanananchi kuweza kujikwamua kiuchumi.
mkuu wa wilaya makete mh juma sweda ametembela barabara ya kinyika- mlondwe na kuona changamoto inayowakumba wanachi wa maeneo hayo na kuahidi kutoa kiasi cha shilingi laki tano kwaajili ya mfuta ya gari litakalotumika kutengeneza eneo hilo korofi pamoja na kuwataka kuweka makaravati katika eneo hilo
hayo yamejiri baada ya wananchi wananchi wa kata ya kinyika wamemuomba mkuu wa wilaya makete mh juma sweda aweze kuwasidia kuondokana na adha wanayoipata ya changamoto ya barabara ya kinyika – mlondwe katika kitongoji cha idofi ambapo mkuu wa wilaya amesema kuwa hatua za utengenezaji ziwenze kuanza kwa kuhakikisha makaravati yanawekwa katika maeneo hayo
wananchi hao mbele ya mkuu wa wilaya katika mkutano uliofanyika katika shule ya sekondari kinyika kwamba barabara hiyo imekuwa ikiwaleatea changamoto kubwa kutokana na mvua zinazoendela kunyesha na kushindwa kusafirisha mazao yao kwa wakati
kwa upande wake kaimu meneja wa tarura ndg kawogo amekiri kuwapo na changamoto hiyo huku akiwata kuwa na subira pindi ambapo jitohada zinazoendela kufanyika ili kufanikisha adha hiyo inamalizika