DC Sweda akagua miradi ya bilioini 1.5 kata ya Ipelele
December 7, 2023, 1:13 pm
Kutokana na fedha kutolewa na serikali ili kufanikisha miradi inatekelezwa katika maeneo mbali mbali dc sweda ameendelea kuhakikisha anafatilia kwa karibu miradi hiyo ili weze kukamilika kwa wakati
Na mwandishi wetu
Mkuu wa Wilaya Makete Mhe. Juma Sweda amewataka viongozi kuanisha miradi yote inayotekelezwa na Serikali na Taasisi mbalimbali kwa wananchi kwa lengo la kuwafanya kujua haki yao katika miradi hiyo na kuleta uwajibikaji katika Serikali kuanzia ngazi ya chini
Mhe. Sweda ameyasema hayo wakati akikagua miradi mbalimbali kwenye Kata ya Ipelele
Pia amekagua ujenzi wa Madarasa na Ofisi Shule ya msingi Missiwa yenye yenye thamani ya shillingi Milioni 120, Shule ya msingi Mafiga ujenzi unao gharimu kiasi cha shilingi Milioni 70
Sweda amekagua ujenzi wa Daraja la linalounganisha kijiji cha Makwaranga lenye thamani ya shilingi Milioni 100 linalosimamiwa na TARURA
muonekana wa daraja linalounganisha kijiji cha Makwaranga
AIDHA mkuu wa wilaya amekagua ukarabati wa mradi wa maji unao gharimu zaidi ya Bilioni 1 na vyumba vya madarasa shule ya Msingi Ipelele unao gharimu kiasi cha shilingi Milioni 250.