Bodaboda Ndulamo wakusanya Milioni 16 kwa mwaka
November 28, 2023, 11:58 am
baadhi ya viongozi wa serikali ya kijiji na jeshi la polisi kwenye mkutano na waendesha bodaboda.picha na mwandishi wetu
licha ya jitihada za serikali kuendelea kutoa elimu kwa vijana kuanzisha vikundi pamoja na kupata mikopo vijana wa bodaboda ndulamo kupitia kikundi chao wameweza kukusanya shilingi milioni 16 kwa miaka miwili ambazo zimekuwa zikiwasidia katika kutatua changamoto zao
na mwandishi wetu
Zaidi ya sh milioni 16 zimekusanywa kwa muda wa mwaka mmoja na wanachama 50 wa kikundi cha wasafirishaji wanaotumia pikipiki maarufu kama bodaboda katika kijiji cha Ndulamo kilichopo kata ya Iwawa
Akizungumza kwenye mkutano wa mwaka wa kikundi hicho katika ofiisi za kijiji cha Ndulamo mwenyekiti Bw Festo mahenge amesema lengo la kuanzisha kikundi hicho ni kusaidiana katika matatizo na furaha pamoja na kukopeshana ili kikundi kiweze kukua na wameweka utaratibu mzuri wa namna ya kusimamia na kuendesha umoja huo ili uweze kuwasaidia wanakakikundi wote katika kujikwamua kiuchumi
Kwaniaba ya mlezi wa kikundi hicho ambaye ni Rabson Mahenge {Mahenge Phamarcy }aliyewakilishwa na Bw Majuto Mbwilo anewapongeza wanakikundi kwa kuendeleza umoja huo kwani kitawasaidia kutatua changamoto mbalimbali na kuwaasa kutumia vizuri fedha walizopata leo kwa ajili ya familia na kuwakabidhi sh laki tano {500000} kwa ajili ya kuendeleza kikundi hicho
mlezi wa kikundi Rabson Mahenge
PC Daulath Jabir kutoka kitengo cha usalama barabarani amewaasa wanakikundi hao kua na leseni na kuacha kuendesha pikipiki bila kuvaa kofia ngumu { helment }kwani hili linahatarisha maish yao na abiria huku akiwataka kufuata sheeria za usalama barabarni ikiwemo kuzingatia alama za barabarani, , kutoendesha mwendoka na kutotumia kilevi
PC Daulath Jabir kutoka kitengo cha usalama barabarani makete
Kwaupande wake mtendaji wa kijiji cha Ndulamo Bi Mariam Cherehani amesema amefarijika sana kuona wameungana kwa ajili ya kusaidiana amewaasa wameendelee kushirikiana na kutoa taarifa ili kutokomeza wizi kwani bodaboda ndiyo wanatuhumiwa kusafirisha vitu vinakua vimeibwa
mtendaji wa kijiji cha Ndulamo Bi Mariam Cherehani
Askali akitoa elimu kwa waendesha pikipiki ndulamo
Makam mwenyekiti wa muungano kijiji cha Ndulamo immanuel amesema kazi ya bodaboda inachangamoto nyingi ikiwemo kuporwa pikipiki na ajari jambo pekee litakalowasaidia ni kudumisha umoja huku akiwataka kuendelea kuzingatia usafi ili kuwavutia wateja
Kikundi cha waendesha pikipiki ndulamo kinawanachama zaid ya 50 na kimetimiza miaka miwili huku kikijidhatiti kusaidiana na kukumbusha sheria za usalama barabara kwa wanachama wake ili kupungiuza ajari za barabarani