Kamishna msaidizi, mkuu wa hifadhi ya Kitulo kuchangia mifuko 10 ya saruji Veta Makete
November 27, 2023, 7:24 pm
kutokana na jitihada za serikali kuendelea kujenga vyuo vya veta nchini imekuwa ni chachu kwa vijana kunufaika na mafunzo hayo katika kujiinua kiuchumi
na shafii
Kamishna msaidizi na mkuu wa hifadhi ya kitulo ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika maafali chuo cha Veta wilaya Makete Theodora Batiko amewaasa wahitimu kukitumia kile ambacho wamefundishwa na kuwa wabunifu zaidi kwenye Yale yote walio fundishwa na walimu wao.
Amesema hayo kwenye mahafali ya 19 ya chuo cha veta wilaya ya makete yalio fanyika chuoni hapo ambapo amewataka wazazi na walezi kuendelea kuwasomesha watoto kwa lengo la kulea familia zao
Aidha bi. Theodora amesema lazima watoto wafundishwe wakiwa bado wadogo huku wazazi wakitakiwa kuwapa nafasi watoto wao kwenye kila wanacho taka kusomea huku akiahidi kutoa mifuko kumi ya saruji kwaajili ya kujenga bwalo la chakula ambalo imekua changamoto katika chuo hicho.
Kamishna msaidizi na mkuu wa hifadhi ya kitulo pamoja na baadhi ya viongozi katika mahafali katika chuo cha veta makete
Mkuu wa chuo cha veta wilaya makete ndg. Elisha Nkuba amesema wahitimu wameandaliwa vyema na hanashaka kwani wana vigezo vyote kuingia kwenye soko la ajira
Aidha mkuu huyo wa chuo amemuomba mgeni rasmi ufadhili wa wanafunzi wakike ambao watajifunza katika chuo hicho kwa kuwa kina miundombinu ambayo inamwezesha mwanafunzi wa kike kusoma.
viongozi mbali mbali wakiongozwa na Kamishna msaidizi na mkuu wa hifadhi ya kitulo katika ukaguzi wa namna mafunzo kwa vitendo yanafanyika katika moja ya darasa chuoni hapo
Nae mkuu wa polisi jamii wilaya makete inspekta Hassan Lujendo amewaasa wanafunzi wano hitimu kuwa makini kwenye Yale walio fundishwa na kuyatumia vizuri
Hata hivyo inspekta Hassan amewaasa madereva piki piki maarufu boda boda kupata mafunzo ya udereva na kupata leseni pamoja na kukata Bima kwaajili ya pikipiki ili kujilinda na matatizo yatakayo tokea kama ajali au kuunguliwa na chombo cha moto.