Kitulo FM

Watumiaji wa vyombo vya moto watakiwa kufuata sheria za usalama barabarani

November 23, 2023, 12:47 pm

Na mwandishi wetu

Wito umetolewa kwa waendesha vyombo vya moto wilayani makete mkoni njombe kuendelea kuheshimu alama za usalama barabarani ili kuepukana na ajali ambazo zinaweza kuzuilika

kutokana na uzembe ambao umekuwa ukifanywa na baadhi ya waendesha vyombo vya moto na kusababisha ajali za mara kwa mara jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani wajidhatiti kutoa elimu wa watumiaji wa vyombo hivyo ili kufuata sheria za usalama barabarani

Hayo yamesemwa na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani wilaya ya makete ndg Benjamini Mwala alipokuwa akizungumza na Kituo hiki  kupitia muendelezo wa utoaji wa elimu kwa wananchi na watumiaji wa vyombo vya moto kuendelea kufuata sheria za usalama barabarani

mkuu wa kikosi cha usalama barabarani wilaya ya makete ndg Benjamini Mwala.Picha na mwandishi wetu

Mwala amesema kuwa licha ya elimu kuendelea kutolewa lakini bado wapo baadhi ya waendesha vyombo vya moto hususani bodaboda wamekuwa hawafuati alama za barabarani

D.T.O Mwala

mkuu huyo wa usalama barabara Benjemini Mwala akiendelea kutoa elimu

Aidha mkuu huyo wa usalama barabara Benjemini Mwala akiendelea kutoa elimu pia amebainisha baadhi ya haki na wajibu wa abiria awapo katika chombo cha moto

D.T.O Benjamini Mwala

kutokana na ajali ambazo zimekuwa zikiendelea kutolea katika maeneo mbali mbali jeshi la polisi kupitia kitengo cha Usalama barabarani Wilaya ya Makete wameendelea kutoa elimu kwa watumia vyombo vya moto ili kuendelea kuepukana na ajali ambazo zinaweza kuzuilika